Busara itawalinda Wasafi ilihali ufahamu utawahifadhi.

Busara itawalinda Wasafi ilihali ufahamu utawahifadhi.

Ya nini makinzano ya kila leo na Basata? (Ulizo). Jema lipo baya lajia nini? (Shangazo)

Lakini Wasafi ambayo Basata hawataki mfanye kwanini myafanye? (Ajabu) 

Lakini wajuzi wanajua ni kwanini kila leo wasanii hawa wamekuwa na mengi yenye kosana na Basata. (Ndiyo)

Wajuzi wanatujuza hakuna kingine zaidi ya ‘Fahari’ kubwa walionayo sasa, ambapo wanaamini yakuwa hakuna wa kufanya lolote juu yao. (Kabisa)

Lakini mswahili nae haachi kutukumbusha kumbukumbu yakuwa “Fahari mama wa ujinga” (Naam)

Vivyo kuendelea kutenda yenye hovyo katika ufahari hakika ni ujinga tu wala msiwe na shangazo. (Uhalisi)

Kwa nafasi zao kwa sasa tulitaraji wao kuwa mfano wa kuigwa katika mengi yenye maana zaidi. (Tofauti)

Basi walau hekima katika usikivu na kufuata taratibu za Basata zikawe sasa juu yenu katika fungulio la nyakati hizi. (Hakika)

Na tunakumbusha tu yakuwa “Kheri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu” (Tafakari)

Lakini pia mnapaswa mjue yakuwa “Uzuri wa godoro nje tu, ndani mna pamba” (Ufahamu)

Sisi tunawatakia yote yenye kheri katika funguliwa lenu la jana juu ya endelezo la muziki wenu na bongo fleva kwa ujumla. (Pongezi)

#MuzikiNiSisi