Busara inamlinda Lady Jaydee na ufahamu unamuhifadhi kwenye muziki.

Busara inamlinda Lady Jaydee na ufahamu unamuhifadhi kwenye muziki.

Wasanii wengi wamekuwa wakipita kiwepesi katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya tangu miaka ya kuchangamka kwa muziki  mpaka sasa 2018.

Na wengi wanapita kiwepesi ilihali wana vipaji vikubwa lakini kukosa busara na ufahamu kumekuwa ni sababu ya wao kupita vyema kiwepesi na haraka.

Licha ya wengi kupita lakini Lady Jaydee ni jiwe kuu ambalo halisogezeki licha ya kuwepo kwa nguvu kubwa ya kutaka kulihamisha jiwe hili kama sio kulitoa kabisa. Lakini wapi kwa hakika jiwe limekuwa na uzito mkubwa kwa upande wa watoaji hodari.

Ni vyema wasanii wapya wajue yakuwa kipaji pekee hakitoshi bali busara kwa maana ya nidhamu lakini ufahamu wa kupembua mabaya na mema katika wakati sahihi.

Kiulizo cha wengi mpaka sasa ni kwa namna gani mwanamuziki Lady Jaydee ameweza kuwepo mpaka sasa? Ilihali wasanii wengi ambao waliibuka katika kuishia mapema.

Lakini ufahamu wa kutoa album nyingi katika muziki umemfanya kuendelea kuwepo kwa maana ya kuwa na uwanja mpana wa kusikiliza. Ni wazi Jide ndiye msanii pekee wa kike mwenye album nyingi kuliko msanii yoyote lakini akiwa msanii wa pili kwa album nyingi katika muziki wote kiujumla. (Album 7).

Itaendelea……..

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa