Bob Junior unataka Diamond Platnumz akubebe mgongoni?.

Bob Junior unataka Diamond Platnumz akubebe mgongoni?.

Kila leo imekuwa Bob Junior akinena mengi juu ya Diamond Platnumz tena katika historia yao hasa pande la lalamiko.

Mara ooh alikuja studio ikawa hivi, mara ooh sijalipwa hata mia ya wimbo wa Kamwambie. Nini hasa unataka katika nyakati hizi?.

Nani anataka kusikia makubaliano yenu katika nyakati za nyuma? au ni kwamba unaumizwa na mafanikio yake ya sasa?.

Kipi hasa unahitaji? au akubebe mgongoni? waswahili hunena “tenda wema uende zako”.

Hivyo wema wako ubaki kama historia nzuri kama wewe ni uzao halisi wa Diamond wa leo hii, lakini lalamiko linasaidia nini kwenye muziki wako?.

Katika kweli yenye kweli Bob Junior amekuwa ni mlalamikaji hodari sasa wa Diamond, na jambo hilo linafanya muda mwingi atoe malalamiko kuliko kazi yake.

Hakuna sababu ya kulalama kila iitwapo leo, bali kazi nzuri na bora ili uweze kuwa kama ambavyo ulikuwa katika nyakati za nyimbo zako nyingi na nzuri.

Na kikubwa utengeneze ufanyaji wa kazi katika karatasi katika kila wimbo ambao utakuwa unatoka Sharobaro Records.

Hakuna haja ya kuonyesha mfadhaiko wako mbele ya mashabiki, maana watu watazungumza zaidi kuhusu fedheha yako na kuacha kuzungumza nyimbo zako kwa upana.

Lakini daima “Kawaida ni kama sheria tu” na ni ngumu kuibadili nyekundu kuwa njano, basi Bob Junior na ajitafakari.

Kwa maana ya kufanya muziki au kuwa mtu wa lalamo katika mfadhaiko wake!!.

#TuzungumzeMuziki