Blog yaweka nyimbo zailizopo kwenye Album ya Vanessa Mdee na watu kupakua bila malipo.

Blog yaweka nyimbo zailizopo kwenye Album ya Vanessa Mdee na watu kupakua bila malipo.

Kwa hakika maendeleo huletwa na mambo leo, kwa maana hali halisi ya ukuaji wa muziki na kasi ya kuwa na blog nyingi katika kuendeleza kusambaza muziki wa wasanii wengi Zaidi.

Lakini katika uwazi kuibuka kwa blog nyingi Zaidi kumechangia kuharibu muziki kwa namna yake. Ingawa ilipaswa kuibuka kwa blog kusaidie msanii na muziki wake lakini imekuwa kinyume.

Na hii imetokana na wengi kutokuelewa namna ya uendeshwaji wa blog juu ya namna ya kipi ukiweke katika blog na kipi kisiweke au ukiweke kwa namna ipi. Na kwa hakika hii ni changamoto.

Money Monday ni album ya Vanessa Mdee ambayo kwa sasa inapitikana katika ngazi ya mtandao.

Na katika ngazi hiyo ni wazi ili uweze kuipata ni lazima ufanye malipo. Lakini tumeona moja ya Blog ambayo ni www.yikaboy.com kuweka nyimbo hizo na watu kupakua bure bila malipo.

Sisi kama wapenda muziki na maendeleo ya wasanii ni wazi imekuwa ni chukizo kwetu kwa maana msanii kama Vanessa amewekeza muda, fedha na akili katika kutengeneza album ambayo ni wazi yafaa irejeshe faida.

Hivyo mtu anapoisambaza bure ni wazi anakuwa anaharibu biashara lakini kuharibu muziki kwa ujumla.

Jambo jema ilikuwa ni blog kusambaza link na sio kuweka wimbo/nyimbo ili mtu aweze kupakua bure.

Tizneez Media Group tunakemea na kulaani vikali blog zote ambazo zinasambaza wimbo, nyimbo,album ya msanii kinyume na matakwa ya msanii husika.

Ni vyema watu wa blog mjue yakuwa “Ulacho ndicho chako, kilichobaki ni cha mchimba lindi”

Picha chini ya blog hiyo ambavyo imeweka nyimbo hizo.

 

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa