Billnass sasa si kelele tena za jukwaani bali ufanyaji shoo.

Billnass sasa si kelele tena za jukwaani bali ufanyaji shoo.

Mara tatu tumewahi nena juu ya ufanyaji mbovu wa shoo wa msanii Bill Nas.

Lakini haikuwahi kuwa chukizo kwake, bali kuikubali kweli yenye kweli na kuifanyia kazi.

Na sasa tunaona namna ya mabadilko yake katika ufanyaji wake wa shoo, sio makelele kama zamani bila kusikika kwa uzuri.

Na hii ni kutokana mtu kama Kacci na kumuweka msanii wake wa sauti za nyuma ni jambo jema mno.

Kwa ambao hamumjui Kacci ni jamaa ambaye alikuwa na Country Boy katika matamasha mengi kwa muda mrefu.

Na uwezo wa kuwa msanii wa sauti za nyuma uliweza kumfanya Country Boy kuonekana bora katika majukwaa mengi.

Sasa yupo na Bill Nas hakika Bill Nas amepata mtu sahihi katika kuwa bora zaidi katika majukwaa mengi.

Shoo ya Ilam ya Arusha Billnas amefanya vyema, pongezi zetu ziwe kwako ndugu yetu.

Kweli yenye kweli imemfanya awe zaidi ya kila leo katika majukwaa mengi.

#TuzungumzeMuziki