Billnas na upendo juu ya Godzilla

Billnas na upendo juu ya Godzilla

Mashabiki wana uwezo mkubwa wakuwapatanisha wasanii ambao huwa hawana maelewano mazuri. Pia Mashabiki hao hao wanao uwezo mkubwa wakuvunja uhusiano wa wasanii ambao wanakuwa na uhusiano mkubwa.

Mambo haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika maisha ya wasanii na kupelekea kuzoeleka kwa hali hii, licha ya kutokutambua madhara ambayo yanabaki kwa wahusika pindi wanapokuwa wanahitaji kushirikiana katika kazi.

Vuguvugu la Billnass na Godzillah lipo kwa mashabiki wa muziki wao na sio ndani ya wasanii husika na mjadala juu ya Billnass na Godzillah bado unaendelea kuanzia Mitandaoni,Vijiweni na Mpaka kwenye Vyombo mbalimbali vya habari.

Hii inachangiwa na aina ya uimbaji wa Billnass kuonekana kupita katika njia za Godzilla lakini Zaidi na Zaidi ni kufanya vizuri kwa Billnass Zaidi Godzilla kwa wakati huu. lakini yote hayo bado yanakuwa yakiishi na kutafsiliwa katika mawazo ya hawa mashabiki wa hawa wasanii.

Kitu ambacho ni kikubwa unachotakiwa kukifahamu ni kwamba Godzilla na Billnas wameishi pamoja na kwa ukaribu  wakati walipokuwa wanasona chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE). Na kwasasabu hiyo kuna uwezekano mkubwa wa Billnass kuwa kuna vitu kadhaa na vya muhimu ambavyo alivipata kutoka kwa Zillah juu ya Muziki wake.

Kwa kuwa wakati huo wako CBE tayari Godzilla alikuwa ana uzoefu wa muziki  na ndiyo alieanza kusikika kabla ya Billnass na pengine ndicho kinachomfanya Billnas asiwe na neno baya au kupunguza upendo wake kwa Godzilla.

Pamoja na kuwepo kwa vuguvugu hili lakini Billnass anazidi kuwa ni mtu wa kutambua fadhila na kutokumshushia heshima kaka yake Zilla ambaye anarekodi nzuri na kubwa katika muziki huu wa Rap hapa nyumbani, na Billnas kufikia hatua ya kutaka kuzirudia baadhi ya nyimbo za mfalme huyo wa sala sala ambazo ni Nataka pamoja na King Zillah. Hapo kunaashilia kuwa Billnass ana upendo wa dhati na Zilla licha ya kuwepo kwa maneno yanayo wazungumzia juu ya muziki wao.

Swala la Billnass kutaka kurudia nyimbo mbili za Zillah hakujamfanya aishie hapo katika kuonesha upendo wake kwa Godzilla kwani Billnass amewajia juu baadhi ya wasanii na mashabiki wanao dai kuwa Zilla ana msongo wa mawazo(stress) na kuwajibu kuwa wao ndio watakuwa na msongo wa mawazo na sio Zilla kwa sababu hawajui anaishi vipi na anakula nini.

Kama inavyokuwa ngumu kuizuia harufu ya marijuana hasa inapokuwa inavutwa basi ndivyo ilivyo kwa Billnass kushindwa kujizuia kuelezea upendo wake juu ya Godzillah.

#MuzikiNiUpendo

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez