Bila umakini nyakati fupi zijazo muziki utakuwa na maisha ya kifo mithili ya Bongo muvi.

Bila umakini nyakati fupi zijazo muziki utakuwa na maisha ya kifo mithili ya Bongo muvi.

Waswahili huamini yakuwa “Hata kufa ni kuishi ilihali ni kuishi katika kifo” hakika ni uhalisi wa uisho wa bongo muvi sasa. Ni wazi ni katika maisha mazuri ya kifo yasiyo na maana katika Dunia ya leo.

Nyakati hizi muziki umekuwa kichaka cha wengi sasa katika uficho wa hovyo zao kwa kivuli cha muziki. Lakini chukizo ni kubwa kwa wasanii wengi wa zamani ambao wa ni wachonga barabara kiasi cha muziki umefika ulipofika.

Wapo wenye kunena hadharani kwa ukubwa bila kujali wala uficho lakini wapo wenye kunena chini kwa uficho. Wakiamini yakuwa wakinena hadharani wataonekana ni wenye chuki.

Lakini sasa imekuwa ni kawaida sasa kuona kila mtu ambaye alitafuta umaarufu nje ya muziki tena katika hovyo kuingia katika muziki na kupewa nafasi kubwa tu. Lakini zungumzo kubwa halitakuwa muziki bali hovyo zake.

Wenye hovyo wengi wapo sasa kwenye muziki, jambo hili linarudisha nyuma muziki maana wenye kufanya muziki kwa upana hawapewi nafasi bali wenye hovyo.

Ni uwazi Ray C kunena yakuwa “Mnaharibu maana nzima ya bongo fleva, achene utani na kazi za watu. Sio kila mtu aimbe it’s bullshit” yuko na usahihi mkubwa.

Ni wangapi tumeona wameingia kwenye muziki na walianza na hovyo zao na sasa wapo na endelezo la hovyo huku wakiwa katika mwamvuli wa bongo fleva? Hakika ni wengi.

Na amini tunenacho yakuwa muziki utakuwa na maisha ya bongo muvi, maana ongezeko la wengi wasio na ujuzi ni kubwa. Lakini licha ya kukosa ujuzi lakini hata nidhamu ya kazi na misingi ya Sanaa pia hawana.

Jambo linaharibu kwa mapana muziki huu, lakini chukizo kubwa ni wasanii wenye uwezo kamili kukosa kabisa muda na kupewa wenye hovyo, hakika bila umakini muziki utaharibika vyema.

Ni vyema wajuzi wa muziki na wadau walitazame hili kwa mapana katika nyakati za sasa kabla hazijaja nyakati za taabu kama bongo muvi.

Daima mswahili hunena yakuwa “Shika shika lingali kichwani” #TuzungumzeMuziki.