Bila umakini mabadiliko ya kimuziki yatampoteza Roma Mkatoliki.

Bila umakini mabadiliko ya kimuziki yatampoteza Roma Mkatoliki.

Katika muziki wa kizazi kipya ni uwazi ulio wazi kuwa wasanii wengi wa kizazi kipya wapo wawili wawili katika tungo, midondoko na mengi yenye kufanana Zaidi.

Ila Tangu kutokea kwa Roma Mkatoliki mwaka 2007 mpaka leo hii 2017 amabaki Roma kama Roma. Hakuna Roma mwingine bali ni Roma kama Roma kuanzia tungo, midondoko na hata maisha yake ya Sanaa na maisha nje ya Sanaa.

Upepo mbaya ambao unapepea vyema sasa kwenye muziki wa kizazi kipya ni mabadiliko ya wasanii walio wengi hasa katika upande wa kurap (Hiphop).

Upepo huu si upepo mwema kwa kila msanii, bali mwema kwa wale ambao waliweza kubadilika na kuweza kutenda haki katika upande huo, ila upepo huwa mbaya kwa msanii anapoenda upande ambao hataweza kutenda haki ya kipawa chake kama ambavyo ilikua awali.

Kuna msemo unaosema “Tunapaswa tubadilike kulingana na mazingira, ila sio kila mazingira yatubadilishe”

Upepo huu wa mabadiliko haupaswi kwa Roma licha ya kuwa nguvu ya ushawishi juu ya wataka mabadiliko ya wasanii wa hiphop ni kubwa mno. Ila umakini na kutizama aina ya soko lake ni jambo ambalo litamfanya aendelee kuwepo na kufaidi matunda ya kipawa chake.

Roma ameweza kuwa bora kwa aina ya muziki afanyao, na ameweza kuwa bora mbele ya wale wasanii ambao wameweza kubadilika. Matumbuizo ni kipimo tosha cha Roma kuwa bora.

Sasa kama wateja wake wanafurahia huduma yake ya kimuziki Roma abadilike nini? Ni wazi mabadiliko ya Roma ni kuboresha Zaidi kazi yake kuifanya Zaidi ya pale alipoishia.

Ila kama Roma ataenda kasi na upepo huu wa mabadiliko ni wazi atakuwa amejichimbia shimo zuri la muziki wake. Maana katika utafiti wetu team tiznez tumegundua mashabiki wa Roma ni mashabiki wenye uhitaji wa uhalisia ule ambao anachana kila leo.

Roma anapaswa kuzingatia hili “Tunapaswa tubadilike kulingana na mazingira, ila sio kila mazingira yatubadilishe”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment