“Bila umakini hakika Diamond Platnumz atawaingiza wasanii wake shimoni”

“Bila umakini hakika Diamond Platnumz atawaingiza wasanii wake shimoni”

“Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” Hakika ni upofu wa mashabiki wengi ambao wamekuwa wakiamini kila neno kutoka kwa msanii wao Diamond Platnumz.

Mashabiki wengi hawajui namna ya kuchanganua hoja, ila hoja zao nyingi hutawaliwa na lugha kali isiyo na maana wala faida yoyote mbele ya maisha yao, lakini siamini kama msanii husika anafurahishwa na mashabiki wa aina hii.

Moja ya kauli ambayo Diamond Platnumz aliisema wiki kadhaa nyuma ni “Sitegemei Radio na Runinga katika kufanya promosheni ya kazi zangu za muziki.

Kauli hii ilizua maneno mengi hasa kwa watangazaji na madj wa Radio na Runinga. Wapo ambao waliamua kutoa mitazamo yao kwenye vipindi vyao, ila pia wapo ambao walitoa mitazamo nje ya vipindi yani katika vijiwe vingi katika makutano tofauti.

Ni wazi huwezi kupinga ukubwa wa Diamond Platnumz katika bara la Afrika na nje pia. Hivyo ana kila sababu ya kusema kila neno ambalo yeye ataona linafaa kwa wakati huo. Lakini je anawaza juu ya wasanii wake?

Ni ukweli usiopingika kuwa wasanii wake ambao wapo chini ya Label yake ya Wasafi bado sio wasanii wakubwa kama vile mashabiki wanavyowajaza sifa wasizokuwa nao. Hawana ushawishi kama wa Diamond Platnumz, ukweli ambao mashabiki wengi huupinga.

“Bora kujikwaa kidole kuliko ulimi” Huenda ni kweli sasa Diamond hategemei Radio na Runinga katika kusukuma muziki wake, ila je vipi kuhusu wasanii wake? Je!nao hawategemei Radio na Runinga kama Diamond? Na aliamua kusema ili iweje?

“Fahari mama wa ujinga” Tangu kutoka kwa kauli yake Diamond Platnumz tuliona hoja za wadau wengi katika mitandao ya kijamii hususani Twitter.Wapo waliosifu kauli hiyo na wapo walioponda kauli hiyo. Na daima hupaswi kupinga mtazamo wa mtu.

Kauli hii imeweza kumtafuna vyema msanii wake Harmonize huku wengine wakisubiri kuona kwa wasanii wengine kutoka WcB vile itakuwa mara baada ya kutoa nyimbo.

Ni siku chache tangu kutoka kwa wimbo wa Nambie wa Harmonize. Ila katika kipindi kichache pia Harmonize hasikiki na wimbo wake licha ya kuweza kumtumia mpenzi wake katika video yake, lakini pia mwanzoni kutengeneza kiki ya kuachana ilhali tu wapate kuzungumziwa ila imekuwa ndivyo sivyo……..

“Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako”

Itaendelea..

Follow Twitter Tizneez

Instagram Tizneez

Facebook Page Tizneez

Youtube Tizneez

www.tizneez.com