“Bila kusoma alama za nyakati n rahisi kuanguka kimuziki” Jay Mo.

“Bila kusoma alama za  nyakati n rahisi kuanguka kimuziki” Jay Mo.

Ulimwengu Ndiyo Mama ni album yake ya kwanza jay Mo ambayo ilitoka mwaka 2002 chini Bongo Record mbele ya mikono ya P Funck Majani. Na hii ni  moja kati ya album bora kuwahi kutokea katika muziki huu wa kizazi kipya. Wimbo kama mvua na jua, bishoo, kama wataka demu, maisha ya boarding na nyingine nyingi zimeweza kufanya album hii kuwa bora wakati wote.

Huwezi kutaja marapa bora wa bila kutaja jina la Jay Mo, ambaye tangu mwaka 2000 alikuwepo kwenye muziki huu wa kizazi kipya. Hivyo mpaka sasa anatimiza miaka 17.

Licha ya upepo wa sasa wa muziki kupeperusha wakongwe wengi lakini tumeweza kumuona Jay Mo akiwepo na akiendelea kupambana kizazi kipya cha rap ambacho ni wazi kina vijana wenye uwezo mkubwa.

Lakini katika kujua kusoma vyema alama za nyakati Jay Mo ameweza kwenda sawa nao. Ni wazi anguko la wasanii wengi wa zamani ni kushindwa kusoma alama za nyakati.

Ni wazi kizazi cha sasa sio rahisi kuelewa tungo za mvua na jua au hata aina ya kurap, hivyo msanii inapaswa ubadilike kulingana na mazingira ya soko la sasa.

Jay Mo ameyajua hayo na ndiyo maana sasa yupo katika uwanja huu wa muziki wa kizazi hiki na anafanya vyema lakini kwenda sawa na damu changa ya kizazi cha mtandao.

Ni vyema wasanii kujitafakari namna ya kwenda na wakati kulingana na wakati husika. Kwa maana tangu kuingia kwa mwaka huu 2017 ni wazi wimbo kama Nisaidie Kushare, Me & you na sasa Tanakula bata ni wazi ni nyimbo zenye kwenda mazingira ya ya sasa lakini zenye ubora.

Hivyo ni wazi Jay Mo lazima afanye vyema kwenye uwanja wa muziki wa kizazi kipya, na wakati wote waswahili husema “Juzi na jana si kama ya leo”

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa