Bila kujua namna ya kutibu tatizo wasanii wataangamia kwa malalamiko tu.

Bila kujua namna ya kutibu tatizo wasanii wataangamia kwa malalamiko tu.

Katika kweli malalamiko hayawezi kuwa mwarobaini wa kutibu tatizo, ilihali pale ukiamua kulifanyia utibabu tatizo husika.

Kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya wasanii wetu wa muziki wa kizazi kipya juu ya Media kubwa, hususani za Jiji la Dar es salaam.

Wengi ni wepesi mno kusema yakuwa tunabaniwa na Media, lakini katika uwazi wanatazama zaidi Media kubwa za Jijini Dar es salaam pekee.

Kwa kutazama media za Dar tu hakika watakuwa ni wenye kujichimbia shimo jema na kutumbukia ndani yake katika kila leo.

Maana katika uwazi wenye kupokea malalamiko hayo (Media) ni wazi hawastushwi wala kufadhaishwa na lawama hizo, bali kuwatazama kwa dhihaka wasanii walalamishi.

Katika kweli yenye kweli na hakika mswahili hakukosea kunena yakuwa “Kilichomo baharini, kakingoje ufukoni” (Tafakari)

Hivyo yapasa msanii husika kuamka kifikra na kutumia media nyingine nje ya Jiji la Dar es salaam.

Ni wazi watangazaji wa mikoani na madj wao hawapesi thamani na wasanii walio wengi, lakini ni wazi hawa jamaa wana nguvu kubwa ya kubadilisha matokeo ya muziki wa msanii.

Jambo jema ni msanii husika kuweka ukaribu wa kazi katika kuwatumia kazi kwa wakati lakini kushiriki vyema pale tu watakapo mahojiano hata kwa njia ya simu.

Hakika twaambieni yakuwa kama wasanii watafungamana vyema na Media za mikoani amini mabadiliko halisi ya msanii yatakuwepo. (Uhakika)

Lakini ni kawaida na kama sheria kwa msanii kung’ang’ana na Media za Jijini Dar es salaam na Media za mkoani kuzipa kisogo.

Ilihali kama nguvu atumiayo katika Media za Dar angetumia mkoani kwa hakika angefikia wengi zaidi.

Hivyo kuna haja gani ya kulalama? zaidi ya kuamka na kuweza kutumia vyema mtandao katika kufikisha kazi zako kwenye Media za Mikoani.

Lakini si mbaya kama msanii akitenga bajeti ya kwenda kufanya mahojiano na Media za Mkoani, hakika jambo hili litamuongezea ukaribu na urafiki wa kikazi zaidi.

Mpendwa msanii amka muda ndiyo huu, malalamiko pekee hayawezi kukusaidia bali vitendo vya kubadilika katika utibabu wa tatizo.

#TuzungumzeMuziki