Basata inabidi yafanyike mabadiliko makubwa kwa sasa.

Basata inabidi yafanyike mabadiliko makubwa kwa sasa.

Daima yasemwa “Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mikono yako kuyatenda. Hakika neno hili hutufanya kunena yale yalipo ndani yetu katika uwezo wetu katika kujenga kesho njema za wasani na Sanaa ya muziki kwa ujumla.

Basata ni Baraza la Sanaa la Taifa ambalo pia ni Shirika la umma na liliundwa kwa sheria ya Bunge Namba 23 ya mwaka 1984.

Ambapo ‘Dira’ kuu ya Basata ni kuwa msimamizi na muendeshaji mahiri wa Sanaa, mapato na uzalishaji wa Sanaa nchini.

Lakini lengo kuu la Basata ni kuwezesha uzalishaji, uuzaji, utumiaji, na ushiriki katika shughuli za Sanaa bora.

Ingawa katika taswira ya hakika kwa wasanii na mashabiki hawaoni dalili wa endelezo la ‘Dira’ na “Lengo’ katika nyakati hizi ilihali ‘Usiasa’

Hakika kilichopo ni usiasa katika endelezo la ‘Dira’ na ‘Lengo’ hakika ni chukizo kubwa juu yao wasanii na mashabiki, na Basata wamejivika upofu na uziwi katika kelele na fujo toka upande wa mashabiki na wasanii.

Lakini kwa uhakika twanena yakuwa kelele na fujo hazitoshi juu ya Basata, ilihali kitakiwacho ni namna ya kupata mabadiliko katika Basata.

Na mabadiliko haya yapaswa yawe makubwa na yafaa watu wawe na mitazamo yenye utofauti juu ya biashara ya muziki.

Jambo kuu ambalo lapaswa kupata mabadilko ni uongozi wa juu wa ‘Basata’. Ni wazi panapaswa kuongozwa na watu nje ya Sanaa husika kwa maana ya watu wenye taaluma ya ‘Biashara’.

Lakini wasanii wawepo katika idara kwa maana yakuwa chombo kipo katika kusimamia Sanaa zote, hivyo yapasa kuwepo idara za Sanaa zote.

Yani kuwepo na Idara ya Sanaa ya muziki, idara ya Sanaa ya uchoraji na nyinginezo.

Na idara ya muziki itahusisha wasanii wenyewe ambapo watakuwa na uwezo wa kuchambua yote kuhusu Sanaa yao, ilihali uongozi ukiwa ni wenye kujua biashara.

Lakini katika kutaka kufanikiwa vyema katika Sanaa yapasa uongozi wa Basata ambao ni wenye taaluma ya biashara uweze kupata fursa ya kwenda mafunzo katika nchini ambazo zimefanikiwa kimuziki ili kuweza kuona na kupata ufahamu kwa namna ipi wenzetu wamefaniki vyema.

Hivyo kama Basata itaongozwa na watu wenye utashi wa Biashara hakika kutakuwa na uwezo wa kutimiza lengo la Basata na Dira. Hivyo Basata itajiendesha yenyewe maana itakuwa ikifanya kazi ya kuuza Sanaa na kusimamia.

Lakini Basata yapasa iwe na kitengo cha sheria juu ya Sanaa “Wanasheria’ hii ni katika namna ya kufanya kazi na wasanii na itasaidia kuondoa mikataba mibovu juu ya wasanii, na kama basata wakipitisha mkataba mbovu juu ya msanii basi hapo yapasa wawajibike.

Lakini mswahili hakucha kunena yakuwa “Shika shika na mwenyewe nyuma” Tafakari.

Itaendeleaa……..

#TuzungumzeMuziki