Barua ya wazi kwa wasanii wote wa muziki wa bongo fleva/hiphop.

Barua ya wazi kwa wasanii wote wa muziki wa bongo fleva/hiphop.

Hakuna sababu ya kukaa kimya kwenye jambo ambalo linaleta maendeleo kwa msanii au hata kwa Sanaa nzima.

Ni wazi wapo wasanii ambao husema “Tizneez ipo kukosoa lakini pia Tizneez mnatumia lugha kali” Hizo ni hisia zao na mitazamo yao, lakini yapasa wajue “Asiyejua maana usimwambie maana”

Lakini pia “Kuelewa ni kipaji”. Ndugu zetu wasanii je! mnajua “Wakati wa hari watu hugombea kisima kimoja?”

Imekuwa ni jambo gumu kwa Team Tizneez kufunga vinywa vyetu juu kuzungumza kuhusu Album. Na tumewahi kuandika .

Hivyo ilikuwa ni faraja kubwa mno kuona Chege ameweza kutoa album yake. Tena ni faraja kuona katikati ya bahari ya kiki na udaku Chege amekuja na kitu tofauti chenye maana kwenye muziki. Ingawa kuna mashabiki wengi hawajui kama Chege ametoa album.

Jambo la kushangaa kwa wasanii wetu ni kuwa kimya kama hakuna cha maana ambacho kimefanyika.

Ni wazi tukirudi wakati mfupi  tu nyuma tuliona wasanii wetu walivyoweza kumzungumzia Jay Z mara tu alivyotoa album yake. Lakini ni wazi album hiyo haikuwa na faida yoyote ile katika muziki huu wa kizazi kipya.

Ila album ya Chege ni wazi inafaida kwa maana kama wasanii wangetumia nguvu ya kumpa muda chege katika kurasa zao ni wazi nguvu ya album ingerudi.

Lakini tupo dunia ya unafiki na ujuaji, ila kuzungumza album ya Jay Z inaonekana ni ujanja ambao katika uhalisia ni ushamba kukataa chako na kusimamia cha mwenzako kisicho na maana wala faida.

Lakini yote ni kutaka ufahari katika kurasa zao ila wakumbuke “Fahari mama wa ujinga”

Umefika muda wa kuthamini vyetu hasa vyenye maana kubwa kwenye maisha ya Sanaa. Yapasa Chege apewe muda mkubwa katika kurasa za mitandao ya kijamii za wasanii kama ambavyo wasanii walifanya kwa Jay Z basi na ifanyike hivyo kwa Chege.

Lakini hata kwenye vyombo vya habari maana katika uhalisia vipo vipindi ambavyo vilitoa muda kabisa kuzungumzia album ya Jay Z na kuweka mijadala. Sasa kwanini vyombo vya habari zikae kimya kwa hili la Chege?

“Hakuna utumwa mbaya kama kutawaliwa kiakili”

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa