“Baraka Da prince ni kipofu wa mitandao ya kijamii hakika atadumbukia shimoni”

“Baraka Da prince ni kipofu wa mitandao ya kijamii hakika atadumbukia shimoni”

Nani ni meneja wa Baraka Da Prince? Je!ni yeye mwenyewe? Ni wazi bila umakini atapita vyema kama upepo wa fukwe za bahari ya hindi.

Ni wazi kipawa alichonacho Baraka yafaa uwanja wa muziki wa kizazi kipya tujivunie vyema, kwa maana ni kipawa cha uhakika na sio cha bahati kama cha wasanii wengine wengi.

Lakini ndugu zetu “Utu busara ujinga hasara” Ni wazi bila nidhamu ni wazi hata uwe na kipawa cha namna gani ni lazima anguko likufike.

Katika uhalisia Baraka hana nidhamu katika matumizi ya mitandao ya kijamii hususani mtandao wa picha ‘Instagram’.

Ni mara nyingi amekuwa msanii wa kuandika lugha kali mbele ya mashabiki zake, lakini hata kutumia muda wake mwingi kuwajibu mashabiki zake kwa lugha kali.

Huku akisahau yakuwa lugha kali hazijengi shabiki bali kumbomoa Zaidi, lakini kujibomoa Zaidi mwenyewe. Lakini kama angejibu jibu vyema kwa shabiki ni wazi angemfanya shabiki huyo kuwa shabiki yake.

Lakini lugha hizi kali ni hakika zinamuharibia picha yake juu ya makampuni kutaka kumtumia katika mambo ya kibiashara. Hakuna kampuni Ambayo itamtumia msanii ambaye hana nidhamu ya matumizi ya mitandao kwa maana makampuni mengi hupenda kutumia wasanii kuanzia ngazi ya mitandao ya kijamii na kwingineko.

Hivyo Baraka ana kila sababu ya kujitafakari vyema. Lakini ndugu zangu yapasa ajue “Mchunga peku hapendi ila hana viatu”

Lakini wakati wote “Hasara humfika mwenye mabezo”

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa