Bagdad umetoa kichwani semi hii au umeagizwa useme na uongozi wa ‘TUMA’? (Soni)

 

Hii ni Semi ya Baghdad kupitia mtandao wa Dozen Selection. Itazame hapa chini

 

Semi hii umetufanya tutafakari yakuwa “Bagdad umetoa kichwani semi hii au umeagizwa useme na uongozi wa ‘TUMA’? (Soni)

Mbona semi imekaa hovyo mno katika tafakari? sasa kama msanii asipokuwa mwanachama atapoteza nafasi ya kuchezwa radioni kwa namna ipi?.

Je! kama akiwa mwanachama na hachezwi radioni chama kitafanya nini?

Pengine hujui acha tukujuze yakuwa Mgosi Mkoloni ndiye Mwenyekiti wa chama hicho na nyimbo zake (Wagosi wa kaya) hazipigwi Clouds Media Group je! imekaaje hiyo?

Na nyakati za Vinega 2009-2010 wote kuanzia Mapacha, Rama Dee, Sugu, Danny Msimamo, Mkoloni, G Solo, Adili Chapakazi, D Wa Ghetto, Peen Lawyer na wengine wengi walikuwa ni wanachama.

Na nyimbo zao hazikuwa zikipigwa Clouds Je! chama kilisaidia nini?.

Na mpaka sasa wapo wasanii wengi tu ambao ni wanachama na nyimbo zao hazipigwi katika radio nyingi je!chama kinawasaidia nini?.

Kama unataka wasanii wajiunge usitoe kauli za vitisho kuhusu Radio maana kuna wasanii kama Nash Mc nyimbo zake hazipigwi na Radio nyingi tu. Hivyo utamwambia nini kama usipojiunga hutapigwa radioni?.

Na hao wasanii ambao ni wanachama na mpaka sasa nyimbo zao havipigwi chama nacho kinataka kuwaombea msamaha kama Media zitakavyo?.

Ni vyema utafakari vyema katika semi, sisi ni waumini wakubwa wa kutaka chama cha muziki wa kizazi kipya kiwe na nguvu, lakini isiwe katika kauli za hovyo kama ulizonena.

Umuhimu ni msanii kutambulika na chama au Basata? Ni wazi ni Basata, hivyo utoe elimisho
la wasanii kuwa na umoja lakini si swala la kusema kutakuwa na zuio la kuchezwa radioni.

Au ndiyo watimiza semi ya mswahili yakuwa “Kinywa jumba la maneno” (Puuzo), Tafakariii.

#TuzungumzeMuziki