Babu Tale na hovyo zenye maana kwa wasio na maana. (Fedheha)

Babu Tale na hovyo zenye maana kwa wasio na maana. (Fedheha)

Wasio na maana wala kujua maana kwao yenye hovyo kuu ni furaha yenye ujazo kamili. Ilihali wenye utashi mkuu ni chukizo kuu. (Soni)

Na mara zote wenye hovyo hutenda wakiwa wanajua, lakini upana wao mkuu ni kuzungumziwa na zunguko la mtandaoni. (Umaarufu)

Lakini kwa wajuzi wakuu hudharau na kupuuza hayo yenye hovyo. Lakini hovyo ya Babu Tale ya kumuita msanii Vanessa Mdee “Malaya” ni hovyo kuu. (Hakika)

Ikumbukwe si kama Babu Tale hakujua anachofanya, bali kufanya kwa kusudi la zunguka ya mtandao wa picha Instagram. (Uhalisia)

Lakini zunguko hili linamsaidia nini zaidi? Ni wazi ni kupata upana wa mahojiano na katika zungumza ya kwake na genge lake katika mengi yao. (Hakika)

Kwa maana kama asingefanya hivyo nani angezungumza juu yake kwa nyakati hizi? Lakini hata kupata mahojiano? (Hakuna)

Vivyo imebidi atende kwa faida yake na genge lake kuu, lakini fedheha kuu ni Vanessa Mdee katika semi ya Babu Tale kwenye mtandao wa picha. (Sikitiko)

Lakini tunakumbuka semi ya mjuzi mmoja aliwahi nena yakuwa “Diamond ni msanii wa nyota tano mwenye nyota tatu begani” (Naam)

Nyota tatu kwa maana mbili uongozi wake ni wenye kuzibeba katika mengi yenye hovyo kuu. Kusaka umaarufu  mkubwa ilihali hauwezi kuwasaidia kitu katika ongoza msanii. (Kabisa)

Kama meneja ananena haya yenye jazo la hovyo mtandaoni, je! msanii wake atatenda yepi? (Ajabu)

Busara kuu yapasa iwe kwa meneja katika ongoza ya msanii kufanya yenye maana katika mafanikio ilihali hekima kuu ikitawala. (Hakika)

Lakini imekuwa tofauti mno katika uongozi wa Diamond, ni kama wamejivika upofu katika hekima. Na tunapenda mjue yakuwa “Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake wote wataangukia shimoni” semi zenye ukuu zanena hivyo. (Daima)

Hivyo tendo la Babu Tale katika semi mbaya juu ya Vanessa Mdee, linakuwa ni tendo lenye kudhihilisha yakuwa “Umri si busara” (Eeh)

Kwa maana hata “Wapuuzi pia huwa wakubwa” Waswahili hunena hivyo katika busara kuu zenye kufunza. (Maisha)

Na inashangaza Babu Tale kujiita mswahili ilihali matendo yake ni yenye hovyo kuu. Ndugu zetu mswahili ni mtu mwenye hekima na maarifa kutoka pwani ya Afrika Mashariki. (Ndiyo)

Vivyo mwenye hovyo na kujiita mswahili mjue huyo si mswahili bali mpuuzi mkuu mwenye upuuzi kamili usio na busara wala hekima za mswahili. (Daima)

Yote ya yote “Utu busara, ujinga hasara” Tafakarii kuu…. #MuzikiNiSisi