“Awali ni awali hakuna awali mbovu” Ali Kiba.

“Awali ni awali hakuna awali mbovu” Ali Kiba.

“Ukweli ni mchungu kama ukiwa umekumbatia uongo” lakini ukweli hutufanya tuwe/uwe huru wakati wote.

Ni masaa machache yamepita tangu kutoka kwa wimbo mpya wa Ali Kiba seduce me, ambapo katika muda mchache uliweza kuchukua mzunguko mkubwa katika mitandao ya kijamii.

Muda mchache tu msanii Diamond Platumz nae aliachia wimbo akiwa na Team yake nzima ya Wcb. Na kitendo hiko kimetafsiriwa na wengi kuwa ni ushindani wake wa kibiashara na Ali Kiba, Na wengi wakionyesha kuchukizwa na jambo hilo.

Na mashabiki wanapaswa wajue jambo hilo la Diamond kutoa wimbo sio dhambi wala baya katika kwa maana ya ushindani wa kibiashara.

Ila uongozi mzima wa Wcb ulipaswa kujua “Mapaka mengi hayakamati panya” Ni wazi hakuwa muda sahihi wa wao kutoa wimbo huo. Kwani tayari wameshasikika kwa upana tena katika upande wa sauti ile ile moja.

Hivyo ni ngumu shabiki kuwapa sikio lao ilihali kuna ladha tofauti. Na daima “Maji huteremka bondeni hayapandi mlima” Lakini waungwana “Mkono usioweza kuukata ubusu”

Hivyo hakukuwa na sababu za msingi za wao kutoa wimbo sasa. Nafikiri kuna haja ya uongozi wao kuwa makini katika mapambano haya ambayo kimsingi huenda yakamshusha hadhi msanii wao badala ya kumpandisha kama wengi wadhaniavyo.

Yapasa wajue “Mshale usio na nyoya hauendi mbali” Lakini “Fahari mama wa ujinga” Na katika uhalisia “Awali ni awali hakuna awali mbovu”  Ndugu zetu ni wazi “Shoka lisilo na mpini halichanji kuni”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa