Angalau viatu vya Albert Mangweair vinamuenea Country Boy

Angalau viatu vya Albert Mangweair vinamuenea Country Boy.

NA John Simwanza

Ni miaka kadhaa sasa tangu alipofariki  mkali wa muziki wa Hip hop nchini Albert Mangwea taarifa za kifo cha Ngwea ziliwashtua wengi na kuwaacha na sintofahamu mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya.

Lakini mashabiki waliamini baada ya kushuhudia mwili wa Ngwea umewasili kutoka Afrika kusini ambako mauti yalimfika.

Mangwea alikuwa ni msanii wa aina yake katika uandishi,Uimbaji, uchanaji,pamoja na utu aliokuwa nao kwa wasanii wenzake lakini pia hata kwa mashabiki wake   ambao walikuwa hawaishiwi hamu juu yake katika kumuona,kusikiliza nyimbo zake pia kuhudhuria show zake.

Albert Mangwea ni moja kati ya msanii aliyewahi kushinda tuzo ya Album bora ya Hip hop ilitwayo”A.K.A MIMI” mwaka 2004, ila pia ni miongoni mwa wasanii ambao wamewahi kutengeneza Hit song nyingi Tangu aanze muziki mbali na hayo lakini Mangwea hajawahi kuharibu au kufunikwa katika nyimbo alizowahi kushirikishwa na wasanii wenzake.

Kizuri ni kizuri lakini chenye ubora ni bora  basi nina kila sababu ya kusema Bidhaa ya Ngwea ilikua ni Bora zaidi na zaidi na kufikia hatua ya kujitambua yeye mwenyewe kuwa ni hakuna kama yeye “Hata kama leo nikifa pengo langu halina spare” Ngwea alichana huo mstari katika wimbo wake wa Speed 120 aliomshirikisha Chid benz.

Nivigumu sana kuziba pengo la mtu flani kwa kuwa kila binadamu tuna uhalisia wetu katika utendaji wa kazi yoyote ile japo kuna kuendana na kuna kufanana katika matendo  na hapo kuna uwezekano wa kumfananisha mtu na mtu kama Ice boy anavyo fanana na 2pac katika muonekano japokuwa utofauti unakuwepo kati yao ukiuchunguza kwa makini.

Country Boy ni msanii aliyeibuka na aina yake ya uchanaji na uimbaji wa tofauti na wengine Uwezo wake wa kupita kwenye midundo ya aina yoyote  umemfanya kujizolea mashabiki na kukuwa kwa kasi kubwa  Ukimsikiliza Country kwa umakini utagundua kuna ladha ya Albert Mangwea hasa anavyo badili flow na jinsi anavosikika akiwa ana rap utapata chembe chembe za Ngwea ndani yake.

Hata katika moja ya tumbuizo alilofanya Country Boy Maisha Club mwaka 2016 Country Boy alionyesha umahiri wake pale alipotuimbuiza ‘live’ nyimbo zake mpaka nyimbo za Albert Mangwea. Ukumbi mzima ulisimama kwa kuhisi ni kama   Albert alikuwa ni yeye jukwaani, na jambo zuri zaidi ni pale msanii Tid alipoamua kupanda jukwaani kuonyesha amekubali uwezo wa Country Boy.

Lakini Uwezo wa Country kuto kushuka kwenye game toka aanze kunaashiria kuzipitia njia za Ngwea,kutoa hit zisizochosha mashabiki ni miongoni kigezo mojawapo na sifa za Ngwea. Ila hata kuwa na maelewano baina ya wasanii wenzake na mashabiki wake nayo inaingia katika sifa za Ngwea.

Ni wazi Country Boy angalau viatu  vya Albert vinamuenea.Kwa kulidhihilisha hilo Country ameifanya vizuri sana Dakika moja aliyoirudia kutoka kwa Ngwea na hapo ndio utakubari kuwa Country bado anaendelea kumuenzi Ngwea kila siku na sio rahisi kusahaurika kama ilivyo kwa wasanii wengine ambao hatupo nao kwa sasa.

Edited by Batro.