Ali Kiba usiende kama Diamond Platnumz nenda kama awali yako.

Ali Kiba usiende kama Diamond Platnumz nenda kama awali yako.

Awali ya Kiba ni muziki pekee katika ujazo kamili. Na hakika imekua vyema maana mashabiki wake ni wenye usikivu wa muziki tu.

Ilihali Diamond ni awali yake ni muziki na matendo katika ushirikishi wa familia yake. Tena ni katika yote yenye kheri ama fedheha.

Yote ya yote hakuna baya kwa maana “Kila mmoja uchagua njia aipendayo katika safari” Vivyo yote ni kheri.

Kitendo cha Ali Kiba kukubali kabisa kuzungumzia familia kwa upana kwenye Media ni jambo lenye chanzo cha mwenendo wa Diamond.

Ikumbukwe ilianza kama udakuu katika upana wa mvurugano wa ndoa yake Ali Kiba na familia yake. 

Kimsingi hakukuwa na sababu kuu ya Ali Kiba kufungua kinywa chake katika eleza ya kila kitu juu ya shutuma za wadaku.

Maana hapo tayari amesharuhusu watu kuendelea kuhoji zaidi. Vivyo baada ya muda itaulizwa tena yakuwa Je! mkeo kasharejea? Vipi maelewano yake na familia yako?

Itapasawa ajibu tena, na ikumbukwe kila jibu huzaa swali. Je! itakuwa ni mwenye kujibu kila leo kuhusu maendeleo ya familia yake?

Na majibu yake yataendelea kufanya walio wengi kufuatilia mke wake na familia yake. Na hii chanzo chake ni yeye kwa maana ameshakubali kuzungumzia hili katika jamii.

Kimsingi ilipaswa aache maswala ya dhihaka katika udaku na kuendelea na shughuli zake, maana kujitokeza hadharani na kusema ya familia yake ni kujipaka matope zaidi.

Lakini daima “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” (Ufahamu). Na hii ilipaswa mno uongozi kushauri katika hili kabla ya mahojiano na athari baada ya mahojiano haya.

Ila yote ya yote itafaa kama atafunga kinywa chake juu ya familia yake na mke, kwa maana hupaswi kujibu kila kitu bali kitu. (Tafakari)

#MuzikiNiSisi