“Ali Kiba ni kutwa mara tatu”

Ali Kiba ni kutwa mara tatu.
Ukimfunika kukata mauno atakushinda kutunga. Ukimfunika umaarufu atakutesa kwa sauti. Ukimsumbua kuhonga media yeye atakuumiza kwa kutojisumbua na hizo media.
Ni kama kumpenda mwanamke ambaye hajui kama unampenda. Na mbaya zaidi hata hisia juu yako hana utaumia sana.
Ndo Kiba hata mashabiki wake wanampenda kuliko yeye anavyowapenda. Anachofanya ni kuwapa kile alichopewa na Mungu. Sauti watu wanadata naye.
Wakati watu wengi sana wakimsifia kwa sauti ambayo anayo yeye tu katika dunia hii. Kuna kitu wanakisahau, ana tofauti sana katika tungo zake sikiliza ‘mapenzi yana run Dunia’
Anamuimbia mapenzi mwanaume mwenzake. Ngumu sana mwenye akili ya kisoda kuelewa ule wimbo.
Mchizi anamuimbia mchizi wake ngoma la mapenzi afu lina bamba mbaya. Hata R Kelly na wenzake akili hii waliikosa.
Dem kaenda kwa Kiba kumshitakia ujinga wa bwanaake. Of coz watoto wa kike wanapenda faraja. Kiba akampa faraja.
Mchizi kugundua kaamua kumtosa mtoto. Mtoto kaamua kutangulia mbele ya haki. Alimpenda mchizi wake ila Kiba alimpa faraja tu baada ya ushauri. Hata mimi ningemfariji kwa namna hiyo mtoto mzuri.
Kasikilize hilo ngoma ukiwa na akili timamu usichanganye na mawazo ya hali ya Wema Sepetu kwa sasa. Hutaelewa alichoandika Kiba.
Kiba siyo wa nchi hii. Kinachofanywa na computer yeye anakitoa kwenye koromeo lake.
Kuna sauti kutoka kooni kwake ni ya pekee kuliko upekee wenyewe. Hawezi kusema ila Diamond na wenzake hicho kitu kinawaumiza sana.
Kiba hajui kujitangaza. Ndo maana hata gari anayotumia haijulikani. Kiba hajui kiki. Ndo maana huwezi kumsikia akiongelea issue zake na madem zake. Hajui kujiongeza ndo maana husikii ana nyumba au shilingi ngapi kwenye account. Na ni ngumu kumkuta news room za udaku. Vyote hivyo hana lakini bado anawaumiza kichwa kundi kubwa la watu. Katikati ya magwiji wa hizi kazi. Fella, Tale na wenzao. Sallam muweke kando hajui fitna za game hili.
Pamoja na lundo la hao watu Kiba bado anasimama nao katika mstari mmoja. Ogopa sana. Heshimu. Hana anachowaweza zaidi ya lile koo lake na akili ya kuandika kinachotakiwa kuandikwa.
Hapa siyo suala la team flan. Ukweli uko wazi kuwa kuna upinzani wa wazi na wa siri kati ya Kiba peke yake na Diamond na watu wake. Huwezi kusikia management ya Kiba ikimuongelea Diamond. Ila ni rahisi zaidi kusikia management ya Diamond ikiongea jambo la Kiba. Ndo ukweli.
Watu wanaomzunguka Diamond huwezi kushindana nao hata kwa nusu saa. Game la muziki liko vyumbani mwao. Linawatii kuliko askari wa Dar mbele ya Makonda. Lakini Kiba kaendelea kuwepo kwenye kilele bila kutumia nguvu. Alichonacho Kiba kwenye koo angekuwa nacho Diamond dunia ingesimama. Ni kama Ronaldo angekuwa na kile alichonacho Messi katika miguu yake.
Mashabiki wanatumia nguvu nyingi sana kupambana na Diamond mitandaoni, wakati Kiba anawauliza wadogo zake vilipo viatu vyake vya michezo akacheze bondeni pale Jangwani. Diamond anajituma sana na muziki wake. Kiba anatufanya tuamini kuwa muziki ni burudani na ufanywe kiburudani.
Wakati soko la muziki likilazimishwa liwe na muziki unaochezeka. Kiba alikuja na ngoma kama Mac Muga ambao hauchezeki na siyo wa mapenzi. ukakamata vibaya sana. Kasikilize Karim. Utagundua kuwa Kiba ni zaidi ya biti na promo.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Imeandikwa na Dr Levy

Attachment