Ali Kiba ataweza umbili mara mbili?

Ali Kiba ataweza umbili mara mbili?

Tumetafakari kwa mapana mno juu ya uhalisi wa Ali Kiba kucheza katika ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa mchezaji wa Coastal Union Tanga.

Na tafakari ni katika semi ya mswahili yakuwa “Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote”. (Uhalisi).

Muziki yeye mpira yeye, je! ataweza vyote? kwa uisho wa mswahili hakika moja lazima limkose kama sio kukosa yote kwa nyakati moja.

Umbili mara mbili ni kazi mno, yani soka na huku muziki kwa upana wa usawia, hakika ni ngumu.

Na katika kweli yenye kweli Ali Kiba kimuziki hajafika mahala pakusema aweze kutulia kwa fanikio kubwa la muziki.

Ingawaje hapa hatujui lengo lake na maana ya fanikio la muziki kwa upande wake yeye tafsiri ni ipi. (Uhalisia).

Lakini katika taswira kubwa ilimpasa awekeze muda zaidi katika njia yake kuu ya muziki. Kwa wajuzi wanaona kwa upana yakuwa umbili mara mbili utamuwia vigumu Ali Kiba.

Ila huenda kucheza ligi kuu ni ndoto yake hivyo yuko katika ukamilisho huo, na hatacheza kwa mapana kwa maana ya kindaki ndaki kwa kila mechi bali mechi kwa uchache.

Kwa maana njia ya ukamilisho wa ndoto yake, lakini uhalisi wa uhalisi umbili mara mbili ni jambo gumu kwa Ali Kiba.

#TuzungumzeMuziki