‘Akili hudhihirika kwa maneno, huthibitika kwa vitendo’ Diamond Platnumz.

‘Akili hudhihirika kwa maneno, huthibitika kwa vitendo’ Diamond Platnumz.

Kila mtu amekuwa na neno lake juu ya swala ambalo limetokea mapema leo katika mtandao wa picha ‘Instagram’ katika ukurasa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz.

Kila mtu amekuwa akitoa hukuma yake kwa namna ya kile alichoandika Diamond juu ya mzazi mwenzake Zari. Diamond ameweka picha ya mzazi huyo mwenzake akiwa swimming ambapo ameandika “Ndio maana wakati mwingine naonaga bora tu nile na kusepa…. maana hawathaminikagi wala kuaminika hawa”

Lakini katika hukumu watoazo watu wanapaswa kujua msemo usemao “Kuhukumu jambo usilolijua hata ukipatia umekosea”  Ila kwa hali ilivyo sasa katika maisha ya kimtandao si rahisi kwa watu kuacha kutoa hukumu kwa maana maisha ya mtandao yanawapeleka watu mbio mno.

Tukitazama katika hoja ya pana swala la Diamond Platnumz kumposti mzazi mwenzake na kuandika alichoandika kwenye ulimwengu wa uelewa sio sahihi lakini katika ulimwengu wa mtandao  ni sawa kwa mujibu wa sasa wa maisha ya mtandao.

Na hapa nasadiki maneno ya msanii wa hiphop Maalim Nash Mc ambapo aliwahi kusema “Vitabu vya Mungu ni ufunuo vya mzungu vitakuvua nguo” Hakika tunaona vile maisha ya ndani ya nyumba yanavyotelewa nje ingawa hakuna sababu ya msingi katika uhalisia.

Lakini jambo hili lina sura mbili, sura ya kwanza ni kiki na la pili huenda likawa lina uhalisia.

Kiki imepewa nafasi kubwa katika hili, ila jambo pekee ambalo anapaswa kujua Diamond hapaswi kutumia kiki kwa ukubwa alionao sasa.

Ila kama ni kiki kama wengi wasemavyo basi tegemea kuona anguko zuri la Diamond kama ambavyo tumeona katika wimbo wa Ben Paul wa wiki kadhaa nyuma pale ambapo aliamua kupiga picha za utupu na kiki kufunikia wimbo wenyewe.

Ukweli uko wapi juu ya hili? Hakika ukweli anao katika kifua chake ila mara zote ukweli huwa wazi muda ukifika, hivyo tusubiri muda utatuambia Zaidi.

Ila katika mtazamo wa wazi jambo hili kama sio kiki pia hakupaswa kufanya alichofanya msanii Diamond kwa maana yeye ni baba na sio mtoto ila kuna wakati busara itumike Zaidi kuliko hasira.

“Utu busara, Ujinga hasara”

Tujiepe muda!Maisha ya mtandao tutaona mengi kwa maana wengi wao hawajui matumizi tofauti na tuonavyo.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa