“Adam Juma Ni jiwe kuu kwenye video za muziki wa kizazi kipya”

“Adam Juma Ni jiwe kuu kwenye video za muziki wa kizazi kipya”
Ni nani shabiki wa muziki wa kizazi kipya asiyefahamu mchango wa Adam Juma katika muziki wa kizazi kipya kwenye upande wa Video? Ni ukweli usiopingika Adam Juma ndiye muongozaji video wa kwanza Tanzania kuleta mapinduzi katika soko la ushindani Afrika.
Kasumba kubwa ambayo imeibuka sasa kwa baadhi ya wasanii, watangazaji na mashabiki ni kuwa waropokaji wazuri tena huropoka hoja nyepesi ambazo hazina mfano wake.

Ni mara nyingi kumekuwa na dhihaka juu ya Adam Juma, Lakini ukitizama kwa umakini wengi ambao huleta dhihaka ni wale ambao walikuwa wakitamani kufanya kazi na Adam Juma miaka kadhaa nyuma.(Wasanii)
Sio jambo baya kulinganisha watu katika kazi wafanyao, ila jambo baya ni kuwalinganisha watu katika mazingira tofauti ya kazi.(Miaka)
Leo hii tunaona wasanii, mashabiki, na watangazaji wengi wakimlinganisha Adam Juma na Hanscana, hivi tunawalinganisha kwa kitu gani?Je mlinganisho upo katika kujenga jitihada za kesho nzuri au chuki? Maana ni vyema kujiuliza mapema hoja hii ya kulinganishwa kwa watu hawa wawili ambao wametoka katika nyakati tofauti kabisa inatoka wapi?

Sio dhambi kuwalinganisha hawa hata kidogo,ila yatupaswa tuwe makini katika kutazama jana zao kwa upande wa kila mmoja. Hapo tutajua je kweli yapasa kuwalinganisha?

Lakini  wakati tunawalinganisha yatupasa tujue nyakati za sasa na zilizopita katika upande wa video zetu kwenye muziki wa kizazi kipya.

Kweli leo tumesahau Adam Juma alipoutoa muziki huu wa kizazi kipya?lakini tusiwe wepesi mno wa kusema fulani ni bora kuliko fulani, bali tuwe wepesi kutazama mazingira ya sasa na nyakati zilizopita.

Ni wazi wepesi wa ufanyaji kazi umekuwa rahisi kwa miaka hii,ila nyakati zilizopita hazikuwa nyepesi kabisa.

Licha ya kuwa ngumu lakini Adam Juma aliweza kuleta chachu ya utamu katika video za wasanii wetu na hata kuweza kuingiza video zetu katika tuzo kama Channel O. Moja ya video ambayo ziliweza kuingia ni Black Chata ya Black Rhino mwaka 2009. Ila zipo nyingine nyingi.

Jamani “Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako”

Aliyoyafanya Adam ni makubwa kwa wakati wake na wakati wa wengi sasa. Na kama tunashindwa kuheshimu mchango wake basi hata Hanscana, Gihcue, Mecky Kaloka, Hefemi, Msafiri Kwetu studio, Nisher na wengine wengi hatutakuja kuwaheshimu maana tunatengeneza vizazi ambavyo havitoi heshima kwa watu ambao walifanya makubwa wakati wa nyakati ngumu za kukuza na kueneza muziki wa kizazi kipya. (Video)

Tufute kasumba ya kuheshimu na kusifu watu mara tu wakishatoweka katika uso wa dunia.

Tumtizame Adam Juma kama chanzo cha video bora nchi lakini pia tuheshimu waliopo na wanaofanya na kuendeleza mazuri kwenye upande wa video.

Lakini pia kwa wasanii ambao wamekuwa wepesi kusema dhihaka juu ya Adam Juma wakumbuke “Akili hudhihirika kwa maneno, ila pia “Utu  busara, ujinga hasara”

Twitter Tizneez

Instagram Tizneez

Facebook Tizneez

Youtube Tizneez