Tanzania pekee ndiyo kuna aina ya muziki ambao sio Biashara

Tanzania pekee ndiyo kuna aina ya muziki ambao sio Biashara.

Muziki ni aina ya sanaa inayotumia sauti mbalimbali za kibinadamu na ala za muziki, huenda ikawa pamoja au kila moja na upekee.Asili ya neno muziki ipo katika lugha ya kigiriki ambapo huitwa ‘mousikee’

Na kupitia sanaa ya muziki msanii huelezea hisia zake au hisia za watu katika mlengo wa furaha au huzuni.Yaweza kuwa kuburudisha au kuelemisha ilihali katika muziki na wajuzi wa sasa kuburudisha ni katika ngazi zote.

Hata katika kuelimisha hakika uburudisho twaupata kwa namna ya msanii kucheza na maneno lakini ala za muziki katika kufikisha hisia za uhalisi kwa hadhira.Na chanzo kikuu cha muziki ni hisia za utunzi wa msanii katika kuwakilisha kwa hadhira.

Na muziki ni bidhaa bora zaidi duniani katika upana wa matumizi ya kila nyakati katika nyakati zote, huenda ikawa huzuni au furaha ilihali kumbukumbu au uhalisia vyote muziki huvifanya katika hali ya utofauti.

Na katika uhalisia wa dunia hakuna muziki usiokuwa biashara bali Tanzania.Tanzania ni mahala pekee Media inaaminisha watu katika uwakilishi wa hisia zao. Ni kawaida na desturi sasa kusikia Mtangazaji akisema “Muziki huu sio biashara”

Ilihali wanasahau yakuwa “Muziki ni hisia” hivyo kusema huu sio na huu ndiyo ni kumpangia mtu katika usikivu wa hisia zake.Na nguvu ya kupangia wasanii ni kubwa, hivyo hatupati muziki mzuri kwa sasa katika kundi la wasanii wengi maana wanapangiwa hisia zao na watu wa Media.

Wasanii leo hii wanalazimika mno kufanya muziki wa Nigeria maana wameaminishwa ni muziki pendwa na biashara, hivyo wanaacha hisia zao na kufuata hisia za kulazimishwa.

Matokeo yake si mazuri maana katika utunzi hawafanyi katika hisia za ndani bali hisia za juu katika lengo la mdau ametaka nini.

Jambo hili linaharibu mno muziki, lakini linafanya tukose nyimbo zenye kuishi katika uwingi.

Ni vyema kila muziki (Hisia) upewe nafasi yake na mashabiki wa muziki wachague hisia zao katika hizo nyimbo lakini msanii kuweka hisia zake za kweli hakika tutasogea kimuziki.

Watu wa Media wabaki kucheza nyimbo kwa upana na si kuwapangia watu yakuwa hii ni bora na hii si bora.

#TuzungumzeMuziki.