Tumemkumbuka Pam D katika siku zake za mwanzo, lakini siku zijazo atakavyopotea kisanaa.

Tumemkumbuka Pam D katika siku zake za mwanzo, lakini siku zijazo atakavyopotea kisanaa.

Jambo baya ni kutosema kweli ambao waujua lakini kushiriki uongo ambao unasifiwa ni jambo baya Zaidi. Na sisi hatuko tayari kuwa sehemu moja na kundi la waongo na wasifu ujuha kwa maana yasiyofaa katika muziki.

Nyakati zote tumekuwa ni watu ambao tunahubiri mema katika muziki lakini kukemea mabaya ambayo yanatokea kwenye muziki kwa maana ya kujenga Sanaa yenye usafi wa muziki mpaka wasanii.

Pam D ni moja kati ya wasanii ambao kuibuka kwao kwenye muziki kulikuwa ni kwa upekee maana mwaka 2012 mpaka 2017 wasanii wengi wa kike wamekuwa ni hodari kwa kuigana katika uimbaji.

Lakini Pam alikuja yeye kama yeye na wimbo kama Nimempata na Popo Lipopo zimeweza kumfanya awe na heshima nzuri mbele ya wasanii lakini kwa mashabiki wa muziki huu.

Ila heshima yake katika mitandao ya kijamii ilikuwa kubwa kwa maana ya kuweka kazi zake vyema lakini kuwa na matumizi mema ya mtandao kwa maana ya kuwekaa ambayo hayana ubaya kwa yoyote yule.

2017 mwishoni na sasa 2018 tumeona kwa namna ambavyo amebadilika mno na kiukweli inashangaza.

Pam amekuwa ni moja ya wadada ambao wanaposti Zaidi kuonyesha mwili wake katika kucheza hovyo ambapo ni wazi si katika kumvutia mtu kisanaa bali mengine yasiolezeka kwa uwazi bali mwenye utashi.

Bila kujitafakari ni wazi anguko la muziki litamfika maana watu watamuingiza katika kundi la wadada wa mjini ambao si wasanii bali kutumia miili yao kwa upana.

Tukitazama nyimbo zake na kusikiliza ni wazi tumekumbuka siku zake za mwanzo za muziki Zaidi si matendo ya video fupi za mitandaoni ambazo kimsingi haziwezi kumsaidia kisanii bali kumtoa nje ya Sanaa Zaidi.

Ni vyema ajitafakari kabla ya anguko jema katika muziki wake maana waswahili husema “Hasara humfika mwenye mabezo”

 

 

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa