JE!!WASANII WA HIPHOP HAWAJUI KINACHOENDELEA?

hiphop-icon

JE!!WASANII WA HIPHOP HAWAJUI KINACHOENDELEA?

Hip hop ni muziki ulionza kushika kasi Tanzania miaka ya 1990 ambapo kipindi hicho kulikuwa na makundi zaidi na sio msanii mmoja mmoja kama ilivyo sasa. Kulikuwepo na makundi yaliyo mengi licha ya machache kuonekana kufanya vyema zaidi na hata kujulikana kwa kasi kadri ya siku, wiki, mwezi na hata mwaka.

Kwanza Unit ni moja kati ya kundi ambalo lilikuwepo, pia kundi kama WWA yani Weusi Wagumu Asilia, Diplomats, Aggly face, Dar young mob,Hardblaters pamoja na makundi mengine mengi.

Sitoacha kusifia hata siku moja juhudi za wasanii wakongwe ambao wamejenga misingi ambayo vijana wengi wa sasa wemeifuata, licha ya watu wachache kutokea ambao ni wazi walivutwa kwenye game na waliokuwepo,(watangazaji na wasanii) licha ya baadhi ya watangazaj wachache kuonekana kutumia nguvu nyingi zaidi kufuta historia za wasanii wengi wakongwe ambao wana mchango mkubwa katika hiphop yetu ya Tz.

Tulikuwa na wasanii wazuri wa hiphop katika kipindi hicho, lakini hata sasa tunao wengi wazuri ambao wameonekana kufanya maboresho mengi hata kufika level za juu zaidi, hakika ni jambo jema maana wanaperusha bendera ya muziki wa hiphop kutoka Tz.

Sitaacha kumpongeza Wakazi ambaye ni kwangu namuona ni moja ya msanii wa hiphop mahiri mwenye uwezo wa kuchana lugha mbili, huyu namfanisha na wakongwe wa zamani, maana wakongwe wengi walikuwa na uwezo wa kuchana kwa lugha mbili yani kingereza na kiswahili. Lakini si kuchana tu hata juhudi za kusukuma muziki wake mbele zaidi bila hata kutegemea media, ikumbukwe hata wakongwe wa zamani walisukumua muziki wao bila media kwa maana nyakati hizo ilikuwa ni ngumu kupata nafasi Radio Tanzania mpaka pale ilipokuja Radio One mwaka 1994 na kuwa radio ya kwanza kucheza Bongo hiphop. Na Taji Liundi ndiye aliyekuwa kinara katika radio hiyo kwenye miaka ya 1994 katika kucheza muziki huo.

Ila katika miaka hiyo 1990 na kuendelea kabla ya Radio za Fm ni wazi wasanii walikuwa wakipeana support kubwa hasa kuanzia kwenye matamasha mpaka nje ya Muziki.

Kauli ya hiphop tunabaniwa haikuanza jana wala juzi, hii ni kauli ambayo mara zote nimekuwa nikikutana nayo maana mara nyingi nimekuwa nikienda kwenye matamsha ya hiphop zaidi , licha ya hayo matamasha ila nilikuwa ni moja kati ya Team The Jump Off iliyokuwa ikongozwa na Jabir Saleh ambapo kazi yangu kubwa ilikuwa na kudeal na washikaji wanaofanya Mixtape uwe msanii mchanga au mkubwa ilikuwa uwe na mixtape tu, basi lazima nikutafute na tupige stori na baadae itasikika katika The Jump off.

Lengo ilikuwa ni kuendelea kusupport muziki huu wa hiphop

Mimi ni moja ya watu ambao siamini kama hiphop inabaniwa isipokuwa naamini wasanii wa hiphop ndio wanaojibania. “Hiphop ipewe muda walau kwa siku masaa mawili tu wabana pua hawatuwezi” haya ni maneno ya msanii mmoja wa hiphop ambaye sitapenda kumtaja jina. Wakati akiongea hayo tayari kulikuwepo na Top 10 ambayo ilikuwa ni ya hiphop tu kutoka kwenye The Jump Off na wengi walipewa taarifa hizo, licha ya Ezden the Rocker, Ncha kali na D7 kuwa vinara wengine ambao ni wazi hawakuficha mapenzi yao katika kusupport hiphop yetu.

Lakini pia The Jump Off ilitoa siku ya ijumaa kuanzia sa 2 kamili usiku mpaka sa 5 usiku kwaajili ya hiphop tu.

Lakini katika hizo top 10 wasanii ambao walisupport jambo hilo hawafiki hata 10 wakati katika uhalisia wapo wasanii wengi kama wangeunganisha nguvu hakika ingekuwa kitu kikubwa. Licha ya kutoa support ya kawaida ila hata nyimbo yake akijua imeingia ni wazi wengi walikuwa wamekaa kimya bila hata kupost katika mitandao ya kijamii. Zaidi ya mara nyingi kuwa watumwa wa kupost nipo radio Fulani ambayo mara nyingi wamekuwa wakilaumu kuwa haisupport hiphop, na hasa wakiwa nje ya Radio hiyo hujikuta wakiongea mengi ambayo hayajengi (Baadhi)

Kwangu nilikuwa naona kama ni kichekesho kama vile vikatuni vya Kaka Masoud Kipanya.

Nasema ninachojua ya stereo akiwa na Fid Q ndio wimbo ninao sikiliza wakati naandika hii makala, wacha niseme ninachojua sasa kuhusu Wakazi

Mwaka jana mwishoni hakika mwaka uliisha vyema kwa msanii WAKAZI, baada ya kuchaguliwa kuwa msanii pekee wa hiphop tokea Tanzania kuwania KORA AWARDS katika kipengere cha Best hiphop Act, kwangu haikuwa habari njema kwa Wakazi peke yake, ili ilikuwa ni habari njema kwa ujumla katika muziki wa hiphop hapa Tanzania.

Lakini katika tuzo hizi pia wengine waliopata nafasi za kutuwakilisha ni Diamond Platnumz, Yamoto Band, Mrisho Mpoto na mwanadada Vanessa Mdee.

Nipo hapa kuzungumzia hiphop maana kupata nafasi kama hizi ni chache tofauti na muziki mwingine toka hapa Nyumbani.

Zoezi la kupiga kura limeanza mwezi mmoja nyuma, ambapo tuliona post kadhaa za kutoka kwa mastaa kadhaa wa hiphop, nakumbuka nilikuwa nikichati na mdau mkubwa wa mixtape Boyca Tamaduni ambapo ni wazi tulisema hii wamepost kutoa noma tu lakini wasanii wa hiphop sio watu wa kupeana support hasa katika nyakati hizi.

Ukweli ni kwamba wasanii wa hiphop Tanzania hawana umoja wenye upendo wa dhati, ila ndani yake wamekuwa wakichukiana wao kwa wao hata katika vitu ambayo vinawahitaji kuwa wamoja. Mfano ni hili la tuzo ya Kora, hakika ilipaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakazi, ili kuhakikisha jamaa anarudi na ushindi nyumbani.

Ni wazi ni kitu kinachotokea sasa, tazama kati ya wale wasanii walio wengi wa hiphop wanatoa support kwa Wakazi?au hawajui kama hii tuzo muhimu katika muziki wetu wa hiphop Tz?

Je!wasanii wa hiphop hawajui kinachoendelea? Kwamba Wakazi yupo katika kupigania tuzo kubwa ya hiphop? Kwangu naona kama ni kituko, sitaki kuamini wala kufikiria kama sasa hiphop umekuwa muziki wa kuoneana wivu, hii ni kwa kile kinachoendelea kutoka kwa wasanii wa hiphop.

Binafsi nilitegemea kuona kila msanii wa hiphop akitia nguvu zake kwenye hili maana wote naamini wanapigania Africa kama sio Dunia ijue, kwamba Tanzania kuna msanii/wasanii wa hiphop wenye kufanya vyema.

Kutia nguvu kuna namna nyingi, lakini nguvu pekee walionayo ni kupost katika mitandao ya kijamii maana sasa watumiaji wa mitandao ambao ni mashabiki adadi yao imeendelea kuwa kubwa, na hakika kama watahimizwa kupiga kura basi ni lazima wafanye hivyo.

Mimi naamini umoja ni nguvu, hivyo ni wakati mzuri wa kuwa pamoja na Wakazi ili aweze kushinda tuzo hiyo.

Kama kweli walikuwa/hukuwa unajua kinachoendelea basi Team tizneez imekujuza wewe msanii/Shabiki kuwa Wakazi yupo katika mchakato wa tuzo za Kora, hivyo unapaswa kutoa support kama mzalendo.

Siku zimebaki chache za kupiga kura hivyo ni vyema kutoa support kwa Wakazi ambaye amepata kibali cha kupeperusha Bendera ya hiphop Tanzania

Sitaacha kumpongeza Dj Tass kwa kuonyesha support kubwa kwa Wakazi, hakika ni mfano mzuri wa uzalendo.

Picha chini Wakazi msanii pekee wa hiphop kutoka Tanzania alichaguliwa kushiriki katika Tuzo za Kora 2016

IMG_6475

Ingawa team tizneez inaamini wewe ni mshindi mpaka hapo ulipofika

Kupiga kura kwa Wakazi Kupiga kura kwa WAKAZI kama Best hiphop Act SmS ”Kora 123″ to +248984000

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez