Kipi ni chanzo cha wasanii wengi kuiga muziki wa Nigeria?

Kipi ni chanzo cha wasanii wengi kuiga muziki wa Nigeria?

Muziki wa bongo fleva unaonekana kukua kwa kasi lakini katika uhalisia ni wazi wasanii wengi wamekuwa wakienda na upepo wa muziki wa Nigeria.

Kwa jambo hili hatuwezi kuutangaza muziki wetu lakini muziki wa Nigeria. Lakini wakati wa miaka ya kuchangamka kwa muziki wa bongo fleva ni wazi tulikuwa na ladha zetu wenyewe ambazo kama tungetumia nguvu iliyotumika na wasanii walichangia kukua na kueneza bongo fleva hakika tungekuwa tunaigwa sisi kwa namna ya muziki wetu ulivyo mzuri.

Haamishi kama wao ni mbaya la hasha! “Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako”

Kitendo cha kuiga muziki wa Nigeria ni kitendo ambacho kinakuwa kwa kasi kila leo, lakini kuna wakati pia wasanii wetu wengi waliweza kuiga vyema muziki wa Afrika ya Kusini.

Mara zote tunasema #TuzungumzeMuziki kwa maana ya kuweka uwazi wenye kusaidia kukua Zaidi kwa muziki wetu. Hivyo tumetafakari ni Kipi chanzo cha wasanii wengi kuiga muziki wa Nigeria?

Na tumefanya mahojiano na watayarishaji wa muziki wa kizazi kipya ambapo kila mmoja alikuwa na maoni yake au mtazamo wake.

Chizain Brain anafungua pazia hili kwa kutoa mtazamo wake.

Msikilize hapa chini.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa