Wakazi ft. Baraka Da Prince – KWANINI (Lyrics)

Wakazi ft. Baraka Da Prince – KWANINI (Lyrics)

INTRO: Life is strange man, maisha ya ajabu sana Unaweza ukakuta mtu anapanga budget ya pesa ambayo mfukoni haipo Yeah yaani unakuta watu wanasemana semana sana Kuingilia maisha ya watu wengine, strange (very) Uuh.. Simatani (Brotha K), Barakah Da Prince, Wakazi VERSE: ONE (Wakazi) Siku haiwezi kupita, bila sauti kusikika Flani amefanya hiki, ilimradi tu visa Kuweka mkazo, kwenye mambo, ya kipuuzi kwanini?! Kusahau yale yote ambayo, ya msingi Yaani kila siku watu hawaishi kunisema Haijalishi hata kama nikifanya jambo jema Mambo mengine mpaka hadi nashindwa kuhema Jinsi walimwengu ambavyo wana nisengenya Mnachokula nyinyi, mimi hakinipeleki chooni Na chooni mlango nina ufunga, hamnioni Iweje upange bajeti na pesa isiyo mfukoni Na kuingilia maisha ya wengine, kulikoni

CHORUS: (Barakah Da Prince)

Kwanini imekuwa, Kwanini katusua, tatizo sijajua Ila Mola ngazi yangu, ushindi imani yangu, mi sitochoka kupambana Kwanini imekuwa, Kwanini katusua, tatizo sijajua Ila Mola ngazi yangu, ushindi imani yangu, mi sitachoka kupambana

VERSE: TWO (Wakazi)

Ni kipi kile kikusikitikishacho Kuingilia ya wengine na kusahau ya kwako Kitu gani, kwani, kama mnene si mimi Maana nikikonda bado mtanizushia ukimwi So all you big girls, you go girls Kuniridhisha sio lazma we uwe model It’s funny, wale ambao maisha yao ndo hovyo Ndio hao hao ambao wanaoongoza kupiga domo “Anaendesha gari gani, mbona anapanda bajaji” “Alizamia marekani au aliishi kihalali” Kila mtu kishageuka Hakimu Mkazi Kiupeo wamefungwa ila ndio wao wa kwanza kujaji

VERSE: THREE (Wakazi)

Nasoma gazeti, eti Hasheem amefukuzwa kwenye ligi Na sheikh, amekula kitimoto siku ya iddi Ya kusema hawana, ni kama, inawabidi Kuongelea ya wenzao, ya kwao, yamewazidi Just wait until its yo turn Lessons of life we all gon learn Y’all been warned, when it all said and done It’s all about you and not no one (Barakah Da Prince) I need freedom kama muimbaji wa Zambia Niwe huru bila mtu kunibania (Wakazi) Hizi ni Sauti za Freedom, Barakah, Simatani, Wakazi Kwanini haya mambo maishani uuh