Sumu Lyrics by Fid Q

IMG-20160814-WA0049

Alieniumba alinipa mdomo hovyo nina haki ya kuongea/ ni bahati nimeotea..safi… Kamwe siachi kuishea/ hamtaki niwe fair…? Trust me.. Me huwa happy niki-care/ na ninaowatouch husema” mshkaji upo smart upstairs / usiache kuongea/ usiache wewe ni incharge huna spear/ kipaji ka ngwear/kwa mpaji ni ka zawadi aliwagea/flag pepea/alihitaji zaidi ya Maji na mmea…? Ilikuaje wamuache hadi mshkaji ulaji wa drags ukamzoea ..?

Tunamoka ili kusafiri kihisia au kufoka pia…ikotoka ukaisikia..huwezi ichoka au kuotosa ikikuingia../ kinachoichosha hii nia…ni kulosa ulichokiota kupatia..kiwachota kihisia…tunasota je inatosha hii fidia..?

Shibe ya mdau hainilazi njaa, sababu mganga yupo juu../ furaha ya baadhi ya wadau ni kuona star anawalamba miguu.

Asie nihitaji simuhitaji, kamwe simuachi anijazie INZI../ bandidu kama TSOTSI sipigi goti kama PNC../ hakuna  ambae hakosi labda ZIZI kwa DEE ANDY../ yangu self esteem haitoki ka riport za TMZ

Na hainizuii nisile mkate kwa kuhofia..kiungulia…/na uemcee hauniachi huniangalia ka fidelia../ka bruce lee hizi karate mtatupigia.. Mtaishia…/na sintosita kusema asante kwa kunisaidia au kuwasifia .. Kwa kunisaidia…

Washkaji baadhi hawana haki ya kuipresha hii medula…/wao wako radhi kukupa pombe na si pesa ya kula….

Nawaona vyura tu kama snura hii sura ya muhuni haina gere…/ mastar wanaovaa masut mtaani nyumbani kunguni tele…

Kwa magonjwa yanayotibika tunapoteza maisha.. Huruma../watachanga kwenye msiba ukifa.. Hawajali ukiumwa..

Au wanaweza wakahisi umekufa kwa kukutwa umezirai…/ usipo stuka Africa unaweza kuzikwa ukiwa hai…

Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji../ ukinizuga kwa ulaji takupa fact kwa lugha ya kiushkaji…

Mnataka vitu rahis..? Me nawapa vitu halis…/ watata mnamtaka ibilisi../na sio huyu big kaka ka idris…

Mrnice jua lanutosi na mtaa unakiu ile mbaya…/ hawamsaport isipokuwa wanawapromoti aliowainspaya…
Wakati ney sio kama moxie STOSHI hakupaswa kumgwaya../ lakini uzee bila noti ni zaidi ya nyoshi akiwa vibaya….

I didn’t come this far just to come this far…/ siwezi sanda kama bikra hata nikiishi kistar

Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unacho tafta…/ pesa ya sadaka wazushi wanaivuta kwa chafu tatu….

Binadam wako wapi hadimnanitoa mie nisiwemo.. / leo nawapa offer ya mswaki halafu kesho mnaning’oa meno..?

Time is money, nafasi haijali kukuzuga../ Wema anataka saa ya almasi ZARI anaujali muda..

Washa sana nyasi, raster yupo kwa fasi vuta../ wanashindwa kujinafas kwa unafki nafsi zinawasuta…

Wabongo wa majuu hamna upendo mnajigawa../ Uongo hauna miguu lakini skendo zinamabawa…

Aliemtia umaskini Africa leo analia kwa yanayomsibu…/ na humtangaza akimpa msaada kiasi cha kumtia aibu…

Dunia sio chafu.. Ni chafu.. Uchafu tukiutazama../ kuna sumu ndani ya watu na hapo hapo tunapokwama…

Hawaamini kwenye kuunda Diamond au KIBA wawili../ wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili…

Cha kupewa hakishibishi.. Ukipewa lazima ukumbushwe…/ Dunia mwendo wa ngisi kung’aa sio lazima star ashushwe..

Ukiacha hisia zikuendeshe Kwa ujeuri utaishia kufeli../ neno la kweli sio zuri na  zuri halina ukweli…

Nitasahau vyote.. Lakini milele tamkumbuka alie niumba../ na daily takaa mkao wa push-up tu  kama Umbwa

 

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez