Ruby X Wakazi – Sijutii Remix (Lyrics)

IMG_6475

Ruby X Wakazi – Sijutii Remix (Lyrics)

INTRO: (RUBY)
Wakaziiiiiiiii
VERSE: ONE (WAKAZI)
Mi ni mchota Maji, nikiwa na kiu niyanywe/Pia ni mvua samaki, nikiwa na njaa niwale/Bahati mbaya, mara nyingi navua kambale/Juu yake misukosuko ya mamba, Pamoja wale/Papa, Kata Ndio inanizamisha Kisimani/Nina Madini Mengi, mtaisikia Kisimani/Nilitupa Almasi na kuokota jiwe nikidhani ni Ruby/Peep the “irony”, Now I’m on a track with Ruby/
VERSE: TWO (RUBY)
Tabu sio kupata penzi/Tabu ni kupata bora mpenzi, mwenye kujua matunzo/Mwenzenu nyuma nilidanganyika kwa kijana/aka nijaze kwa sana/Si Ndio nikaona hili Ndio bwana/Nilizama pasipo zamika, Ona nikadidimizika/Ila sikujali nilijipa moyo nikamuomba mungu/Mbele ya safari nikajipa Moyo nitampata Mzuri tu/MwenZenu nyuma, ooh yeah/Mwenzenu nyuma, ooh yeah/Wacha niseme Maana yamenifika shingoni/Nakosa unene Amani sina moyoni/
CHORUS: (RUBY)
Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi/Wacha niseme Maana yamenifika shingoni/Nakosa unene Amani sina moyoni/Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi eeh/Ooh eeeh nimejifunza Mengi eeh (Wakazi: Life lessons)
VERSE: THREE (RUBY/WAKAZI)
Mto wenye mamba wengi/(Wakazi: yeah) Ndio huo huo wenye samaki wengi, inabidi niingie nivue/(Wakazi: hamna jinsi it’s the only way to do it yo) Mwenzenu nyuma, nilidanganyika na kina/(Wakazi: Tell em girl) Nikajazwa kwa sana si Ndio nikaona nimepata/Nilizama pasipo zamika, (Wakazi: All that glitters is not gold) ona nikadidimizika/Ila sikujali (Wakazi: I experienced that) nilijipa Moyo nikamuomba (Wakazi: I got a story to tell too) Mungu/ mbele ya safari nikajipa Moyo nitampata Mzuri tu/
VERSE: FOUR (WAKAZI)
Wanasema natakiwa kuoa haina shida/Ila shida ipo kwenye kumuoa nani, isiwe kuiga/Mi na yeye nilidhani tungekuwa Beyoncé na Jigga/Naflow ka Jay-Z, bae ni Bey kwa kuimba/Ila mchumba ana mapana ya tembo, marefu ya twiga/Maringo Kama ya paka, na kisirani Cha Simba/Yeah I’m a beast I know, Ila sio kwa this beauty/Who would sleep with all who told her she’s a cutey/Hakujua anachotaka so alichukua anachopata/Bila kujua uzuri wa msichana hupungua kila mwaka/Wanazaliwa wapya, na wazuri hawajazaliwa/Omba Mola akupe mpenzi wa dhati, others, majaliwa/Penzi langu halitaki, anataka tu tuwe washkaji/Kisa bado muziki haujanilipa sina hata bajaji/Au akinionjesha penzi nisiseme iwe Siri diih/Amenifunza Mengi, kumfahamu sijutii/
CHORUS: (RUBY)
Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi/Wacha niseme Maana yamenifika shingoni/Nakosa unene Amani sina moyoni/Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi eeh/Ooh eeeh nimejifunza Mengi eeh