RAFIKI – Izzo Bizness (Lyrics)

Bado ni ngumu Kusadiki / Yupi Rafiki na Yupi ni mnafiki mzandiki / Nasimama imara niko fit/

Nawapima watoto hizi level hawafiki / Nimesimama wima sitoki niite Kisiki/ Ubishi ni ule ule

hata kama sisikiki / naamini kwenye Mungu mimi siziamini Kiki/ 2017 wamebaki na tahamaki/

Coke Studio kaenda Izzo? Wanauliza kivipi/ mishangao kibao wameshikwa na taharuki / Mentali

sina noma naperuzi peruzi Kurasa tu nawasoma/ hawajui ni Baraka toka kwa Baba na Mama/ na

huwaga mimi sichoki kuongea na Maulana/ wana-fake ile mbaya wanajifanya wana/ wameshika

makali furaha yao kutuchana/ tabasamu na mahug feki tu tukikutana/ Mioyoni chuki kibao

mabaya Kuombeana/

(Chorus)

Yupi Rafiki?

Kwenye Shida kwenye raha zama zote yeye atakaa

Yupi Rafiki?

Hawezi kudanganya haamini kwenye Hasi anaamini kwenye Chanya X 2

Kwenye shida kwenye raha ni balaa Rafiki wa kweli atakaa kwenye matatizo shida na dhiki

hakimbii kama Motor Car X 2

(Verse 2)

Rafiki wa kweli ni nani bado natafakari na jibu halipatikani/ wa kwenye raha tu kwenye shida

haonekani/ wa kwenye afya tu magonjwa yuko mitini/ wa kwenye bata tu matatizo ni yangu

mimi/ wakushinda vijiweni/ kutwa kunifitini/ tafakari na mimi/ Yupi wa kumuamini/ ni kweli

haina ubishi / wengi hawamaanishi/ vichefuchefu kibao vyanzo vya matapishi/ Mungu baba

nipe upeo niweze kuwajua/ yupi real yupi fake niweze kutambua/ yani yupi haina kwere yupi

anazingua/ na kwa hili dundo tu najua washajijua/ Nakamua ile ki-GWM/ watoto wa kiume

tabia za Ki-demu/ Kung`ata Kupuliza yani kila sehemu/ Ndumi la kuwili ndio lao nickname/ it’s a

Shame nawashangaa Godamn/

(Chorus)

Yupi Rafiki?

Kwenye Shida kwenye raha zama zote yeye atakaa

Yupi Rafiki?

Hawezi kudanganya haamini kwenye Hasi anaamini kwenye Chanya X 2

Kwenye shida kwenye raha ni balaa Rafiki wa kweli atakaa kwenye matatizo shida na dhiki

hakimbii kama Motor Car X 2

Yupi Rafiki… Yupi Rafiki… Yupi Rafiki….