Parapanda Lyrics By Rostam

Intro
Wanamiliki visenti,
Mambo yamebuma mipango haisomeki
Kuna manabii fekii,Ramani hakuna kila kitu hakielewekii
Parapanda italia parapanda
Parapanda italia parapanda

Lyrics1:
NYERERE:Karibu Mzee kingunge,kwenye makazi ya milele
Mi huku na mji wangu,tayari unaitwa Nyerere
Nimeshtuka kukuona huku,nini chanzo cha msiba?
KINGUNGE:Ni mipango ya mungu,na nimekumiss swahiba
NYERERE:Vipi nchi yangu mtawala ni chama gani?
KINGUNGE:Bado ni CCM ingawa kuna upinzani
NYERERE: Unamaana gani,kwahiyo Rais ni nani?
KINGUNGE:Rais ni John,ndio anaongoza usukani
NYERERE: John Mallecela?
KINGUNGE:No,Magufuli,ulimwacha ni mbunge wa chato sijui unamkumbuka vizuri?
NYERERE: Aaah!ngoja kwanza,unajua haya mambo haya,
Mi nilidhani alipotoka Mkapa angefata Jakaya
KINGUNGE:Jakaya alitawala,akaja akaretire
Nimeacha mengi,yani mambo ni moto,mambo ni fire
NYERERE: Aa’aaa!mbona naskia kama hali haiko sawa
Na ni akina nani hawa,ambao wanajiita ukawa?
KINGUNGE:Ni wapinzani walioungana, lakini hawakumshinda magu
Wengine chama walihama,na bado wakapata tabu (sana)
Kakomesha ufisadi,(kodi)kaongeza ukusanyaji,hakika wamepata mkomboZi ambae atawafikisha nchi ya ahadi
NYERERE: Niliskia skuizi bunge halionyeshwi kwenye TV
Inamaana hoja za viongozi wananchi haziwafikii
Na Mitandao ya kijamii je vipi haiwasaidii?
KINGUNGE: Kuna dada anaitwa Mange,please hide my ID

Chorus
Wanamiliki visenti,
Mambo yamebuma mipango haisomeki
Kuna manabii fekii,Ramani hakuna kila kitu hakielewekii
Parapanda italia parapanda
Parapanda italia parapanda
Lyrics2:

NYERERE: Je vipi kaburi langu,tayari wamelijengea?
Na vipi kuhusu mke wangu,Maria wanamtembelea?
KINGUNGE: Kuhusu kumtembelea,hilo toa shaka
Wanamjali na kumlea,tena kwa heshima ya mamlaka
NYERERE: Na nimemuona shemeji yangu,ama kweli mnapendana,mmefatana
Penzi la kweli kufa na kuzikana
Vipi mwanangu Makongoro,mali zangu anazichunga?
KINGUNGE:Bora wakwako mwenzie busy na Tunda
Hivi Julias ulikua simba au yanga?
NYERERE: Kiukweli niliipenda yanga,ila simba ni kisanga
KINGUNGE:hahaa!mwalimu unajua hadi kisanga
NYERERE: Acha hilo naskia mengi,kibamia hadi kudanga
KINGUNGE: HahaHAa
NYERERE:Na nimemuona komba huku,nyimbo za chama anatunga nani?
KINGUNGE:Mi naskia wataisoma namba ila sijui ameitunga nani?
NYERERE: Sijakuelewa kwani anaesimamia sanaa ni nani?
KINGUNGE:mmmh! lipo baraza ila wasanii wanaishi uani

Chorus
Wanamiliki visenti,
Mambo yamebuma mipango haisomeki
Kuna manabii fekii,Ramani hakuna kila kitu hakielewekii
Parapanda italia parapanda
Parapanda italia parapanda

Lyrics3:
NYERERE: vipi kuhusu muungano bado upo au umechuja?
KINGUNGE: Mpemba anauza kariakoo,na mzaramo ana duka unguja
NYERERE:Ujinga,Maradhi,Umaskini bado maadui nipe kaifa?
KINGUNGE: Ujinga angalau,hao wengine janga la taifa
NYERERE: Kuhusu barabara?
KINGUNGE: zipo
NYERERE: Madaraja?
KINGUNGE: Yapo
NYERERE: kama vipo ina maana uchumi umepanda eenh
KINGUNGE: Wadai cherehani mbili ukiwa nazo una kiwanda
Vyuma vipo still na hospitali hazina vitanda
NYERERE: Bado na maswali mengi vipi mwenendo wa katiba
KINGUNGE: Mchakato ulisitishwa inasemekana walimpiga
NYERERE: Walimpiga nani?na ni akina nani,na ninani alifanya?
KINGUNGE: Mwalimu sijui ila ni watu wasiojulikana
NYERERE: waliompiga risasi Lissu?
KINGUNGE: ni watu wasio julikana
NYERERE:na ni akina nani waliomteka Roma?
KINGUNGE: ni watu wasiojulikana
NYERERE: na wanaoteka waandishi wa habari
KINGUNGE: E eeh!sijui ni watu wasio julikana, hahahaa….

Chorus
Wanamiliki visenti,
Mambo yamebuma mipango haisomeki
Kuna manabii fekii,Ramani hakuna kila kitu hakielewekii
Parapanda italia parapanda
Parapanda italia parapanda.