P THE MC – MITAA NAYOTOKA ( LYRICS)

Verse One:
Natoka mtaani ambako birthday chache MINGI MISIBA/
Mtaani ambako hakuna raha NYINGI NI SHIDA/
Elimu sio kigezo kwa demu MSINGI NI FIGA/
Na hakuna mnyonge hata ukimkuta DINGI NI NIGGA/
Mchana mpaka USIKU vyote NOMA/
Usiombe ukakutana na mbwa MWITU kwenye KONA/
Wanakupukutisha kila KITU huku UNAJIONA/
Na utulie maana usipoanzisha TIFU ndo UMEPONA/
Matozi PIA WEZI/
Wakiharibu chimbo chaka bovu WANAJICHIMBIA MWEZI/
Mchana WANAJISKILIZIA STENDI/
Ukiwatazama jinsi wanavyovaa hata KUWASINGIZIA HUWEZI/
Masuti na MATAI kama BOSI/
kumbe nuksi hao ndo HAWAFAI ni MIKOSI/
Jicho nyanya washavuta DRY kichwa MOSHI/
Wengine wameshapoteza mpaka UHAI kwa KUFOSI/
Wangapi ni MIFUPA ndani ya UDONGO? / (wangapii)
Wangapi WAMEKUFA wana USONGO? / (wangapii)
Wangapi WANAJUTA kuwa WABONGO? /
Washa hustle sana life haiwi SUPA hata KIDOGO/
CHORUS:
Mitaa nayotoka (scratches. . )  bom bronx/
Ki – Kiwalani. . .  yeah/
Mitaa nayotoka (scratches. . . ) bom. . . . bom bronx
Ki – Ki – Kiwalani. . . Yeah/
Verse 2
Mtaani kina mama WANAPANGA BAMIA/
Wengine mboga kichwani WANATANGA NA NJIA/
Bize na biashara KUZICHANGA RUPIA/
Wakati watoto wa mafisadi WANAMWAGA MABIA/
Biashara zetu ni Karanga,  PIPI UBUYU/
Kivipi tusifunge vibanda UKIPITA USHURU/
Wengine washazamia South AFRICA kwa mkaburu/
Kwetu giza nene Mungu nakuomba MULIKA NURU/
Maninja WANAKESHA TU, muda wote PRESHA JUU/
Vita na mamwela sababu ya kusaka PESA TU/
KitaELEWEKA TU,  na wataCHEKA TU/
Shida leo ukishashikwa mkwanja life DEJA VU/
Vijana hawaendi SKULI WANARANDA/
Vibegi mgongoni vina MAPURI ya GANJA/
Vagi lao dakika SIFURI tu UNASANDA/
Hawasomi na wanapiga hesabu NZURI kwenye MKWANJA/
Huaga tu INAFIKA TIME,  naamua KUANDIKA RHYME/
Kuhusu real life iwe mtaani ama INSTAGRAM/
Mbali NTAFIKA MAN, deals NITA SIGN/
Nyingi na kwa nguvu ya Mola wangu daily NITA SHINE/
Repeat chorus. . .

Attachment