Mzee wa meli lyrics Artist; Meddy samurai, Producer; Mas Stanza

FB_IMG_1447851412598

(Intro)
Yeah!
Meddy Samurai
Mas Stanza.
Mzee  Meli
Mbwa Wakali Minyoro Mibovu
Indisputed Record

Verse 1

Alianza kama utani..
Ebwana ntasafiri ndicho alichosema akiwa maskani..

Safari tumezoea..
Hakutaka kutuambia anaenda wapi tukabaki kungojea..

Safari ya kujinadi tukahisi ni ya mbali wasiamini wakabaki kumzomea..
Kwa kuwa ni mchizi wangu wa karibu nikahisi sina haki ya kuongea..

Akawa ananiambia twende ferry..
Mara kurasini kumbe ana mipango ya kuzamia kwenye meli..

Mpango wake sikuamini akataka ibaki siri kati yangu tu na yeye..
Hata nyumbani wasielewe..

Na anasema ana uhakika ata-win..
Kama week mchizi alitembea nakumbuka ilikuwa miaka ya tisini..
Japo nilishuhudia akipanda meli lakini nilibaki sikuamini..

Mwana atafika ama atabaki!!..
Nikabaki na mashaka ndani ya nafsi..
Moja mbili hazikai au watamtosa kwenye maji ili aliwe na samaki..

………Chorus……..
Mzee wa meli..
Bye bye mzee kwa heri..

Verse 2…

Miaka nenda rudi..
Hakuna hakika ka ulifika na lini utarudi..

Barua tulizoandika zimebugi..
Kuzituma kazi bure hatujui ulipokwenda europe, america ama uarabuni..

Jitihada zimefanyika..
Watu wanaomba dua kama uhai.. hata barua basi andika..

Mzee wa meli, mama watoto amekumiss..
Watu wanajiuliza ama ulidandia meli ya wagiriki..

Siamini kama kweli ninachosema..
Hivi ni kweli haupo tena..

maana siku zinakatika na watu wanasafiri..
kabla siku haijakatika najiuliza mara mbili..

Ni nini kimefanya ukapotea?
Kwa nini haukutaka kukaa chini tukaongea?..

Najua ni baraka kwenda mbali kutafuta..
Lakini sio haraka ulioiacha umetuacha tunahaha kuchwa kutwa..

……….Chorus……….

Mzee Wa Meli..
Bye bye mzee kwa heri..

Verse 3..
Salamu zinakuja baada miaka kukatika..
…yeah..
Ni kama miaka kumi na tisa..
Tushasoma visomo na arobaini ila wala hatujazika..

Sana inahuzunisha tunavyosikia..
Umefanya Familia inanung’unika na kulia..
Wakitazama picha zako zilizotumwa huko insta zinatishia..

Ujumbe uliowatumia wanao umewafikia…
Umewataka wasihadaike na safari za dunia..

Usia.. na mumtunze mzazi wenu..
Tanzia.. dunia njia najua me nakufa ila mnikumbuke baba yenu..

Biashara iliitika..
Nimezunguka hii dunia peru’ colombia’ asia na america..

Naona baridi mwili mzima nateseka..
Umebaki huzuni mbele yangu siwezi hata kucheka..

Nimebaki mtu mzima siwezi hata kuchonga..
Kilichobaki huku china bado mwezi tu kunyongwa..