Mwana FA-DUME SURUALI (Mashairi)

Artist: MWANA FA
Song: DUME SURUALI

Hudat hudat hii ni salam na ufahamu
Kama unauza mapenzi sio kwa binam
Hakuna haja ya kusubiri hii ni hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja kama askari wa zamu
Dume suruali Dume kaptula
Shauri zako mradi sipati hasara
Usione utani me sihongi hata kwa ishara
Utaniambia nini mpaka unigeuze fala
Kwanza nasikia hongo zinaleta mkosi
Sentano yangu hugusi Hata ukiongea kidosi
Yabaki mapenzi tusileteane ujambazi
Hata upige sarakasi Utachonga Viazi

BAHILI KAMA NINI!!!!!!!!!

Ndio mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

Nihonge nanunua nini kwanini yani
Kuna kipi nisichokijua ina TV ndani
Usiulize ntakupa nini dada piga moyo konde
Viuno vingi kama mwali wa kimakonde
Usipende hela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate zako
Vishawishi vingi binti sema na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu wako
Tajiri mtata kama Salah
Zipo ila sitoi me ni balaa
Unapenda hela zangu nami nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake bye baby tutaongea

MWANAUME WA HIVYO WA NINI SASA!!!!!!!!

Ndio mnavyosem
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema
Aje aje ajeeee Me mtoto fulani ghali
Nihonge gari Ma swt swt baby
C u to day unipeleke part
Aje aje ajeee Njoo nikupe TBT

Sio kwa enzi ya Magufuli
Zali ilikuwa long siku hizi hakuna la mentali
Nikikuhonga na ukiniacha nitakujia usingizini
Naepusha shari matatizo yote ya nini
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nisiyyafanya nishayasikia
Ningekuwa mhongaji ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani wote wangekuwa maadui zangu

MWANAUME HOVYO WEWE!!!!!

Ndio mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

Baki na hamu zako

Hata pantoni lina staff