Mtazamo Remix Lyrics by Baghdad Faet Nikki Mbishi &Donkoli

Mtazamo (Remix)

Artist Baghdad Ft Prof Jay, DonKoli & Nikki Mbishi
song : Mtazamo
Prod : P Funk

 

Yeah..

Akha

Ekhee

Yoo

kOkho kokho kho

vers 1 DonKoli

Hiki kizazi kimevurugwa na hapa kazi
tupe dili wapi adili nataka kuchapa kazi

Old school new school vibe
wakongwe walinukisha si tunazirudisha vibe

Ninani anaetisha si tumetisha zaidi ya babu
tunaendeleza hi sanaa na tuna nyingi tu ghadhabu

Ghadhabu?

Yes ma underground tunafanya rap inang’ara
media zinaboa wanavyotufanya mafala

Tumechoka ku hustle mipauko chini ndala
na hatujala usiku kazini nyie mmelala

Nyie mmelala!

Tukopesheni promo tupige mikono
tugonge vitu vinono ili wafunge iyo midomo

Darasa hili somo piga mishono
hivi vitu havifundishwi darasani kama ngono

Dundo hili kali kitambo lililisumbua
siku hizi mc mkali eti video inatusua

Counsues mc ana sifa za kubana pua
una sound sexy ^
hizo sio zangu kampe makamua

Kuna mtu anaenijua, mi bingwa wa kuzibua
Eti mweusiii!
washamba mnapanda meli ya mabua

Mnahema mkipanda mkishuka tu mnapumua
wengi mnalindwa na irizi mi ndo nalindwa na dua

Game imejaa majipu koli nayatumbua
chunusi kausha niache mi ni dili na surua

 

Chourus

Ni mtazamo zamo mc usiogoe kivuli

Bora ukemee mabaya na usifie mazuri

Ni mtazamo zamo mc usiogoe usikwepe umande

Okoa sanaa ya bongo ili uchume upande. *2

 

Ves 2 Baghdad

Game imeshakuwa ya wadau
Tale ana nguvu ya kufanya media house zikudharau

Kama hauna hela jiunge mkubwa fela
Lasiiivyo utaendelea kuwaimbia masela

 

Dj kakusaport wiki mbili we ndinga
Mkikutana leaders vinywaji anazinga

We unatungua vya chidi mapenzi mwenzio ana winga
Na raba ya buku 5 akhsanta mmachinga

 

Siku hizi shabiki anaamuliwa
Bando na vocha ananunuliwa

Kina kasanula wanasujudiwa
Niko nyumbani davido anapeta nabaniwa

 

Imetosha sasa tumebeba sana unga
Shida yetu ni mchele tubebesheni mpunga

Tunaowapa utajiri tunaishia kujidunga
Mola wasamehe wanakubali kuwa mapunga.

 

Kama unapata moja kwaa nini usipatee na mia
Hiyo inawezekana kwa wote mlio na nia

Sioni sababu za msingi kuomba kwenye mitaaa
Kama unakipaji iweje ufe na njaa

 

 

Chourus Prof Jay

Ni mtazamo zamo mc usiogoe kivuli

Bora ukemee mabaya na usifie mazuri

Ni mtazamo zamo mc usiogoe usikwepe umande

Okoa sanaa ya bongo ili uchume upande.

 

 

Ves 3

Niko ghetto namsikiliza Nash mc Zimaaa
nikimimina juice ya mango gaden na fina

Huku natafakari kesho ya tasnia
sa skia ushkaji ndo mtaji na cash pia that’s clear

Simuoni wakunishinda
wajinga mpaka mgongwe radion ndio mpushi ndinga

Nauza mitandaoni mtaani unuki chinga
nachafua hewa na baada ya shuzi kimbaa
Yeaaa

Ama kweli bongo ladha bongo lala
wengine kwa sababu hamjafika mwitongo labda

Kwa baba wa taifa kukusanya blessing
ndugu fanya upesii, harakati huku kama jeshi

khaagh…..

sanaa yetu imezorota
basata boroka mashaka ni kwa cosota

kitambo, tuliipiwa bila mipango
wezi wamerudi tena round hii wana mitambo

Yule usimuache ruby achuje
salam kwako mh nape ndauye

Mnapenda aslai sa iwaje muwatenge nyuki
huu ni wangu mtazamo jamaani masela msijenge chuki

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez