Mchumba Lyrics By Logic

BETI 1

Back in dayz nilimuona mama/
chuo kikuu dodoma nikahisi kumpenda sana/
nakapanga mikakati ya dhati awe wangu wa haki/
baada ya masomo ndo tuishi bibi na bwana/
ratiba zake ngumu akiwa free yuko town/
napewa namba yake napiga hapatikani/
Kashanipaga stress  kushinda chumbani/
kwakua ni mpenda shule nitamwona darasani/
nilipomwona cafe nilitamani nimwambie/
msosi alioagiza ni tayari nimlipie/
Niseme nampenda dunia nzima na usikie/
yuko na tag lake ma ustadhati ma bibie/
mwanaume hachoki mwanaume hakati tamaa/
lindoni nikawa makini zaidi ya simba mwenye njaa/
bila kumpata haijakamilika furaha/
nakahisi kudata /
mshamba nikiachwa kwenye mataa/

KIITIKIO

Nataka nikuambie mchumba we ndio wangu unaenifaa/
Nataka nikuambie mama mi ndio wako ninaekufaa/
Hata kama kuna yule jamaa Tafadhali Achana nae/
Mi ni meli kwako nimetia nangaa usinimwage ujikatae/

BETI 2

zikazuka tetesi  yuko resi na dunia/
hata town anakokwenda kuna shefa anahudumia/
Ndo mana hana shobo anaringa anajisikia/
ma boyz wa chuo kikuu hatuna story kumwambia/
hivyo hana nafasi moyo wake umejaa/
mshika dau mkwasi mwili wake kautwaa/
habari mbaya hizi nazidi kuugua kichaa/
mantiki wa uhakika mdomo wazi naduwaa/
nikatamani kumchukia sizitaki mbichi hizi/
kumbe ni wivu tu nikimtazama simmalizi/
ana mwendo wake  alafu macho kwa wizi/
ama zangu ama zake nikimpata simbakizi/
mwanaume hachoki mwanaume hakati tamaa/
lindoni nikawa makini zaidi ya simba mwenye njaa/
bila kumpata haijakamilika furaha/
nakahisi kudata /
mshamba nikiachwa kwenye mataa/

KIONJO

Ni kama naota vile uko nami /
kusema naogopa utanimwaga mami/
Ukweli nimechoka kuuweka moyoni/
Mapenzi mape-mapenzi mapenziiiiii/

KIITIKIO

Nataka nikuambie mchumba we ndio wangu unaenifaa/
Nataka nikuambie mama mi ndio wako ninaekufaa/
Hata kama kuna yule jamaa Tafadhali Achana nae/
Mi ni meli kwako nimetia nangaa usinimwage ujikatae/

Beti 3

ndani ya 18 mi na kipa Men A/
amekubali wito je maneno atakataa/
anaonekana mpole  ka mlokole huyu kifaa/
anavyojali muda basi mkononi ana saa/
nikamweleza nnavyohisi si ibilisi/
nnachojua ni upendo unanituma nikushawishi /
bila we sio rahisi huu sio mwili wangu halisi/
nimepungua sana stress juu yako haziishi/
aliuinua uso machoni chozi anatoa/
akauliza unataka harusi au  unataka ndoa/
moyo wangu sio mweupe wajinga wameutia doa/
kama utaweza nikupe mi sadaka najitoa/