Maneno ya shabiki Lyrics By Nikki Mbishi

Maneno Ya Shabiki
Lyrics:1
Nikki Mbishi ana chuki ana wivu ana ghubu/
Muziki umemshinda hana kitu anatubu/
Anaishi chumba kimoja anajitia kiburi SUGU/
Fid alisema hana nidhamu mithili ya Willy wa Dudu/
Stress zimemjaa ye” ni pombe tu na ndumu/
Game imebadilika ye” anakomaa tu na ngumu/
TV zimemchoka na redio zimemtosa/
Anapost tu mashairi kweli soko limemnyoosha/
Wenzake wanapiga mchele kimya kimya bila kwere/
Wana magari tele na majumba kama mbele/
Kazi yake kupondaponda hana fact wala mantiki/
Anaota kuna siku atasaniniwa na ATLANTIC/
Anajidai mjuaji hapendwi hana washkaji/
Hana tuzo wala taji nini benz au bajaji/
Kifupi jamaa mzugaji mamluki msindikizaji/
Anatuletea uzushi anadai uhai ni maji/

Lyrics:2
Alijifanya anaacha muziki njaa ikazidi akarudi/
Ana-diss kutafuta kiki hapo ndipo anapobugi/
Kipaji Mungu kambariki tatizo hafanyi juhudi/
Ukimwambia ukweli anaku-block hana budi/
Anaita wenzie ma-wack redioni hana hata hit song/
Nahisi anavuta unga maana ushkaji na King Kong/
Duke mwenyewe hasikiki si apige ngoma na Ring Tone/
Abba na Mr. T-Touch wanaotawala kingdom/
Ya production,apunguze harakati/
Muziki umejaa corruption na ye” RUSHWA hataki/
Wenzake wanaachia ngoma zina-trend kwenye chati/
Daily wana-take over Kwake airplay ya manati/
Haendi na wakati hana swagga pale kati/
Umri unazidi kwenda na ametengwa na kamati/
Anaendekeza ngenga sijui atajenga wapi/
Anashindwa na Dogo Janja sababu anapenda unafki/

Lyrics:3
Ukiacha Sauti Ya Jogoo hana tena album kali/
Videos zake zote mbovu wenzake wanasikika mbali/
Muziki umemuacha chali siku hizi anauza mistari/
Tangu enzi za JK haalikwi hata futari/
Ya Ikulu,itakuwa vipi usawa huu wa MAGU/
Sanaa haimlipi hata aseme aende kwa babu/
Anajiona special wakati maajabu hana/
Asipofanya commercial “ATAPATA TABU SANA”/
Maana kipigo chake ni zaidi ya cha Mr.Nice/
Jinsi alivyofulia hapati hata Insta likes/
Akitaka tumkubali ajipange aje tena/
Laa sivyo hasikiki tena hadi Mange akisema/
Aache bangi akiitema hapo brand ataijenga/
Apate manzi kama Nandy amfanye ka” Billnenga/
Nikki Mbishi Nikki Mbishi Nikki Mbishi kitu gani/
Mwenzake wamewasha “MO FAYA” hamuoni kitu hewani/

Written/Composed by @nikkimbishi #2018