Mafanikio Lyrics By Fid Q Feat Baraka Da Prince

Fid Q feat Barakah The Prince – Mafanikio Lyrics intro: Barakah The Prince kila mtu anataka mafanikio.. verse 1:Fid Q Kujisikia nipo juu mie sitaki hizo deals/ sipendi makuu hivyo nitabaki kuwa real../ na kila track ya Q aaah,.. ni wazi utaifeel/ ni wazi iko full aah MZAZI ninakill/ ninamwagika kama Masika../ ninaheshimika na sio kanjibai/ kwa huu mziki wa bajaji hadi kwa washkaji wenye macadillac/ unawashika ile kibabylon.. unauzika sana maghetoni/ ilimradi tu wawe happy more..midadi tu ila party noooo/ mkisinzia mtaniudhi nishawapa vyeo/ tuwape wapuuzi waliodai hii haiuzi haya matokeo/ safari ni hatua.. kufika inabidi uianze/ haina kukita au kusita.. inabidi ukaze/ ingia, ongoza au fuata njia, kukimbia ni mwiko/ kuanzia ulipo sio sawa na kubakia ulipo/ nikisema ‘chini hapana’ nina maana fanya unyanyuke/ na ukiamini umesimama mwana.. komaa usianguke/ ukijituma na neema inakaribia../ nyuma walio-give up mapema wangekaza wangeifikia/ penye… happy.. jitusu.. unafki usiuruhusu/ yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu/ kibongobongo longolongo shazi/ endelea kusaka mchongo hata ukipata kazi/ HOOK: Barakah the prince Tunachukiana? ndio../ ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio/ ongeza mbio/ sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio/ haukungoji wakati.. ooh wewe/ zinapita nyakati..ooh wewe/ muda wako bahati.. oh wewe/ verse 2:Fid Q Na kughairisha kisa haupati sapoti/ ni kujificha na kuuliza giza.. iko wapi ile tochi?/ haupati ile noti/ na wakati wa ule uboss ushapotea/ hautaki ukose? usiache ofcoz endelea/ utafanikiwa kwa unachojua au unachofanya/ wachache ndio hutusua kwa jinsi tu wanavyoonekana/ mafanikio hayaji ukikata tamaa../ yenyewe huwafuata wanaojituma na wale wasiosukumwa na njaa/ sipigi kila dili mipaka imezingatiwa/ sitaki kuwa tajiri ninataka kufanikiwa/ ili kuheshimiwa kwanza ni lazima ujiheshimu/ lakini kufanikiwa ni maujanja tu sio lazima elimu/ ili kuyadaka wengine hugeuka wabaya/ mafanikio kwenye kuyasaka wengine hugeuka malaya/ hugeuka was(i)o haya/ kutwa utawakuta kwa babu/ na anayefanya mambo ya maana huwa hana muda wa kuyahesabu/ kwenye kuyasaka hakikisha haufilisiki/ haupotezi maisha au vile vitu havinunuliki/ sio kama hatucheki kwasababu tumezeeka?/ nope.. ni tunazeeka kwasababu hatujawahi cheka/ HOOK: Barakah the prince Tunachukiana? ndio../ ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio/ ongeza mbio/ sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio/ haukungoji wakati.. ooh wewe/ zinapita nyakati..ooh wewe/ muda wako bahati.. oh wewe/ utumie basi… eeeh eeeh/ bridge: Barakah The Prince una mpenzi (na) uko lonely?/ im sorry ndugu.. haujafanikiwa/ maisha ni kama boli, magoli ndio kufanikiwa/ oooh ooh oooh..oooh.. ndio kufanikiwa/ kila mtu anataka mafanikio…/ outro:Barakah The Prince hhhmmm.. hhhhmmm.. oh mafanikio oh mafanikio kila mtu anataka mafanikio