Lyrics mpya za Nikki Mbishi ni moto

Verse 1:

Ng’ombe apigaye kelele ndio apewaye majani/

Agomapo ng’ombe wa mbele wa nyuma yu matatani/

Wakubwa tu mashakani sembuse wafugwa ndani/

Miti yote huteleza ndo muda wa kufa nyani/

Wa kushauri nani kwa kauli na lugha gani/

Utapewa kesi ya uchochezi na kuitwa mvunja amani/

Mungu kanipa mtoto cha ajabu hakuja na sahani/

Nisipojitutumua atakaye mpa kula nani/

Suka kwenye usukani/

Safari ya Tanzania unaweza shuka njiani/

Mola shusha hisani wakora kutwa ibadani/

Kwa bastola haki inaporwa nyufa ukutani/

Viroba navyo noma ni kama ukutwe na mjani/

Bangi chocho gizani lakini rizzla dukani/

Zinalipiwa kodi makato yote kwapani/

Miundo mbinu inajengwa kwa hisani ya wamarekani/

 

Verse 2:

Mheshimiwa sijachanganyikiwa kiakili/

Sio wote waajiriwa wengine tumejiajiri/

Makatili wamekatilia mbali/

Mirija ya mapato ya wajasiriamali/

Kazi mbovu wanataka pongezi kwa lazima/

Wana pepo inafaa wapate maombezi ya Gwajima/

Najua hatutofika kwa kukosoa kosoa/

Hata fidia msipolipwa tunabomoa bomoa/

Miksa donoa donoa chinga funga biashara/

Ukinyang’anywa robota la mitumba si hasara/

MC ninayejiamini sipangiwi cha kuchana/

Kama ambavyo Mhe. hupangiwi cha kufanya/

Haupo juu ya sheria na sijakushurutisha/

Nafsi yangu imeniambia nije kukuburudisha/

Usikumbatie wabaya na kuwaonea wema/

Kama burudani haitoshi basi nitarejea tena/

 

Verse 3:

Wanahabari mpo huru pengine wekeni pozi/

Kumbukeni Mwangosi na kisha mfute machozi/

Mkiona kimenuka geukeni Ma-Harmorappa/

Kimbilieni kwa Sabuka kabla Ammo hazijawaka/

Wa chini tunachekesha kwa kuwa juu mnaboa/

Mi nina vyeti vya kuonesha vipi mkuu wa mkoa/

Sijali umauti unifike napaza sauti nisikike/

Hivi hujasikia fununu za kuhusu Daudi Bashite/

Mashaka yangu ni utendaji wa BASATA/

Upendeleo mwingi na ujengaji matabaka/

I’m Sorry JK imepigwa pini kapuni/

Ili hali Wapo ya Nay imempa kiki uspuni/

Sitarajii tena kuitwa central/

Naomba mnipuuze mnione kama mento/

Malaika tutaishi kama shetani/

Na shetani ataishi kama malaika,tumeisha/

 

By @nikkimbishi 2017