Lyrics: Haikuwarahisi Song: Haikuwarahisi Artist: Maarifa BigThinker ft DudySound

song: haikuwarahisi

artist: Maarifa BigThinker ft DudySound

verse 1

nilishazibwa mdomo na waliotaka buku aongee/

hadi kwa gubu/ vurugu/

niendako nisifike ila tu walisahau bwashee/

nirahisi kumuosha maiti shughuli kufanya atembee/

nilishazugwa na record’deal na sikurekodi chochote/

utadhani nimeibiwa cocaine sikushitaki popote/

nilijihakiki kivyovyote nikiamini siku zote/

Airtel yatosha ila MUNGU hutosha yote/

sa nikakaza nikikumbuka uuh/

vile kwakuwa nisugu ‘mista’ nitaibuka tuu/

vile nikawaza sipaswi badili nia/

nlishaulizwa utatoka lini hata kabla sijaingia/

nilifahamu kipi nawinda/

sikuhofia kuitwa mjinga/

maana uwoga wa mabaya pia ninjia ya kujilinda/

wapo walionipinga kwa hila ila sikuweka mjadala/

maana ni ngumu kumuamsha aliyejifanya amelala/

chorous:

eeeeeeee eiiiiiiiiiee  ningekuwa na kichwa kidogo lingenizidi sikio

oooh.. ooh… ooh… oooooohhh…!!  ningetaka kuishi kinafki ningekuwa mjumbe ndio

eeeee …. eiiiiiiieeeeeeeee…. haikuwarahisi  oooh..!! ooh… ooh oooooh.. haikuwarahisi

sijafika niendako ila hata kuwa hapa haikuwarahisi

verse 2

nilikaza haswa naninachokipenda/

ningefata uzuri wa barabara ningepotea ninapokwenda/

nilikaza hata walipoita hii kazi sifuri/

maana isemwayo kazi mbaya sio sawa na mchezo mzuri/

nilikaza kibishi mikiki haiishi/

nilichohitaji siku nikifa mjue kwanini niliishi/

makini nilihisi mwisho nikaamini ninao waaminia/

wanasubiri nipotee kisha waniambie wanaijua njia/

{mmmhh} mtanisamehe lakini/

ningefanya mtakacho nitakacho ningefanya lini/

mngefanya nyinyi/ juu chini ningefanya mimi/

mwisho wa stori ungesikia jamaa atafanya lini…..??/

kwahiyo nilibaki mwenyewe/

nilicho dharau ni dharau yenyewe/

muhimu niliona kujifunza ndipo nilijuwa/

bora kuchelewa kuliko kuwahi nisipo pajuwa/

chorous

eeeeeeee eiiiiiiiiiee  ningekuwa na kichwa kidogo lingenizidi sikio

oooh.. ooh… ooh… oooooohhh…!!  ningetaka kuishi kinafki ningekuwa mjumbe ndio

eeeee …. eiiiiiiieeeeeeeee…. haikuwarahisi  oooh..!! ooh… ooh oooooh.. haikuwarahisi

sijafika niendako ila hata kuwa hapa haikuwarahisi

verse:3

kwakuwa mchongo ni mziki/ mziki na mziki/

unamengi kale mpaka kizazi hiki/

bila imani hufiki nakupa na hili/

ukiwa jogoo na hauwiki unaweza kufa kwa utitiri/

umri sio hoja nilijiamini tangu mdogo/

nilipoona mlango mkubwa ulindwa kwa kufuli ndogo/

bila zogo kusema nao sikutoka povu/

wanafki wapo kama nzi utazama tu ulipo ubovu/

mpaka leo nachora/

nilianza kuwa na mawazo mengi kabla ya kuwa na mawazo bora/

nahata waliosema kuwa sitoongoza/

wanaona haya zaidi ya aliye jamba huku akitongoza/

chuki imewaponza iliponiongoza dhamira/

sina hila nina juhudi nahii dhamira/

yangu dira/

cha maana kukuaga fikra/

sikudata a ujana maana hata bibi alikuwaga bikra/