Lyrics By Nikki Mbishi

Lyrics:1
Nilikuwa kituoni nikingoja daladala/
Nikamuona manzi mmoja akivuka barabara/
Viatu mchuchumio na Ana mdomo ka chuchunge/
Nikaona kwanza nivunge ningoje mpaka avuke/
Mkononi Ana mkoba mwekundu bastola nundu/
Sikuwa na mapepe nilikuwa nimepoa kizungu/
Hakuna aliyenishuku kituoni sikuwa mwendaji/
Kumbe mwendawazimu Mission Town Mbumba Mpigaji/
Nimenyuka nimevunja duka mavazi/
Mfukoni mboli imetuna kizushi kumbe makadi tu/
Na attitude /
Ya utanashati ili mradi tu/Udwanzi mtupu na siachi MTU/
Nikamgusa bega la kulia/
Wakati huo kushoto amegeukia/
Unajua nini ilifuatia/
Nikamnyang’anya alichoshika/
Akapiga kelele za mwizi umati ukaitika/
Wengine na vitofa vishoka vigoda/
Sauti za tumuue tumuue zikasikika pamoja/
Akatokea jamaa si ndo akahoji kwanza kisa/
Nikawaambia Mi sio mwizi ila mwizi ni huyu sista/

Lyrics:2
Haikuwa rahisi kueleweka/
Wananchi wenye hasira wanahisi kunifyeka kuniteka kuniSILA/
Nikiwa nimemshika mkono asiponyoke/
Jazba kibao natusi kizungu japo ndo broken/
Nikawaambia wazee kwanza naomba mtulie/
Huyu dem hamfahamu ngoja story niwapatie/Ilikuwa Mombasa nyamaza Dada usilie/
Siku ile beach na wenzako mkaniomba niwanunulie/
Mitungi na misosi na swimming niwalipie/
Muogelee mpige picha kwa Insta mkazitupie/
Baada ya bata ndefu nikaomba uniachie /
Namba yako nikitoka baadae nikupigie/
Nikupitie tukalegeze chaga we na mie/
Kipi kilikufanya shetani likuingie/
Baada ya mapenzi dawa ya usingizi unipulizie/
Uniibie Mali zangu na kisha unikimbie/
Mtoto mzuri Kama Wewe unafaa hata kuwa mbunge/
Unaishi kwa utapeli maisha mguu ndani mguu nje/
Najilipa hii pochi simu na pesa zake/
Zote alizonazo nasepa na asinifuate/

Lyrics:3
RAIA wakashusha zana zao zote chini/
Ghafla wakamchenchia yule Dada wa watu maskini/
Kwa kuwa niliongea kwa hasira na kujiamini/
Wakamponda sista duu mzima na kimini/
Unajitia mjanja umeibia mtoto wa mjini/
Ya mwizi ni siku moja siku hizi si arobaini/
Mwana kakuchaisa na kisha kaingia mitini/
Oya jama tuondokeni alie analia nini/
Ukweli ni kwamba hakuniibia/
Ule ni mchezo tu ambao nilimpangia/
Ukiniona mtaani kaa mbali/
Nitakupora hiyo SAA ya mshale/

By @nikkimbish 2018

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa