Kunywa maziwa Lyrics By Nikki Mbishi
KUNYWA MAZIWA Hook: Aisee tunywe Maziwa /
Ukiacha vumbi vipi mimoshi tunatumia/
Najua nyote mnanisikia /
Na kama ikiwaingia msikose kunywa MAZIWA /
Lyrics:1
Sigara nyingi glass moja ya Maziwa mwisho wa mwezi /
Wakati kwa siku unavuta paketi tatu za fegi/
Unaharibu mapafu ndugu yangu ipende afya/
Kunywa maziwa unaweza ukaepuka cancer ya ghafla/
Makuli kariakoo shimoni vipi/
Jitahidini msikose hata lita mbili kwa wiki/
Maana Kuna kifua kikuu TB mziki /
Ushasikia jamaa alichomwa sindano sixty/
Ni risky Maskini gongo Tajiri whiskey /
Tunaunguza maini na kuhusu maziwa mtiti/
Kwetu Musoma mifugo ya kutosha/
Ukiacha Ziwa Victoria maziwa ni ya kuchota/
Ukikosa Fresh kunywa mtindi usikonde/
Ya dukani mengi feki hakikisha ni ya ng’ombe /
Tena wa kienyeji yamethibitishwa utatisha/
Usishinde mgodini halafu hunywi utakwisha/
Si ni mammalian hatufundishwi kunyonya/
Maumivu ya vidonda vya tumbo maziwa yanaponya/
Unapita na jagi uswazi wanaponda/
Eti anakunywa maziwa daily na bado amekonda/
Ukinywa sumu unapewa maziwa/
Huoni kiasi gani maziwa yamebarikiwa/
Mobimba ya mama inashauriwa /
Kwa watoto mpaka miaka miwili sijapatia? /
Lyrics :2
Dada mwache baby anyonye maziwa /
Kama unavyonya koni nisome my dear /
Ukiacha hizo lengo langu ni kuteta na wahuni /
Wanaopasua mawe Tegeta kutega uchumi/
Namuona bibi yangu anafagia barabara /
Na vitendea kazi hafifu saa saba mchana/
Jua kali hana ndala wala buti sio uzushi/
Atakunywa vipi maziwa na ujira bull sh*t/
Pesa za madafu hela mbuzi/
Hujakunywa Maziwa tangu juzi we si mpuuzi labda mchuzi/
Excuse me naomba kombe kubwa usiweke sukari/
Wakati wa Ramadhan yanashuka hata na ftari/
Napenda Maziwa /
Bila kunywa ni Msiba uliotenga wafiwa/
Hawasemi ananyonya wanasema mtemi kazaliwa/
Somo ni kunywa MAZIWA na ndio Mada inayokaziwa/
Ningekuwa Rais ningesambaza bure/
Kwa watoto wote wa mitaani hata wa shule/
Watoto taifa la kesho vijana taifa la leo /
Watunzaji ranchi za taifa msitafune pembejeo/
Tutakosa mifugo Maziwa na vitoweo/
Maziwa huniweka fresh ninachowaza ni maendeleo /
Tanganyika, Nyasa, Victoria yote Maziwa /
Baada ya hiyo misokoto msiache kunywa MAZIWA /
#KunywaMaziwa Written /
Composed by @nikkimbishi 2017 ********#KUNYWA_MAZIWA *