“Kuna Nini? /Ndani Ya Ile Nyumba” Lyrics By Nikki Mbishi

“Kuna Nini? /Ndani Ya Ile Nyumba”

Written/Composed by @nikkimbishi 2017
Lyrics:1
Ni jengo tu jeupe lenye uzio na walinzi/
Alojengewa mwana anayeaminika kuwa mshindi/
Wa kura za uchaguzi walizopiga wananchi/
Walio dai kuibiwa na bado neno hawatamki/
Linagombaniwa kutwa kucha/
Kwa mitutu na Rushwa/Watutsi na Wahutu wanakufa/
Juilize hawa wazee hivi ni nini wanatafuta/
Mjengoni miaka 40 ina maana hujakikuta/
Babu alisisitiza lile sio Pango/
La walanguzi,fisadi jiweke kando/
Uongozi ni karama utashi usio na gharama/
Wapo wenye roho safi na wenye nafsi za kinyama/Kama
Adolf Hitler mnazi wa Ujerumani/
Kasi ya kazi izidi ila tusirudi utumwani/
Mzee wa nukuu wapi ajifiche uso/
Tumuombe Mungu Tanzania isifike huko/

Lyrics:2
Watoto wa nyumba hii wanachoma nyumba ile/
Hekima zao ni Sawa na za Teacher Mpamire/
Tunagombana Panzi kunguru wanatucheka/
Ile saa unajieleza kwa UHURU ndo wanakuteka/
Mbinde na migogoro kusaka mamlaka/
Hata ushibe Makongoro huzikwi na Madaraka/
Wa nini vibaraka ma C.I.A/
Ama kweli This Is Africa ‘T.I.A’/
Mpaka viongozi wa dini wanapenda ile nyumba /
Zaidi ya Mbingu inayowafanya mnanena hadi kwa lugha/
Amani kwa Mugabe,Museveni na Kagame/
Bila nyie wake zenu nyumbani watabaki wajane/
Mwambieni na Kabila na Nkurunziza wakaze/
Wakitaka hata wakae milele basi tuwaache/
Cheo dhamana mabosi wanaamashauzi/
Kila mtu anaota kucheza na wale Tausi/
Wa ile nyumba.. Lyrics:3
Kuwa yule mwana sio Rahisi kama kuperuzi udaku/
Kuna wakati wasafi Wanacheza na wachafu/
Ukitawala muda mrefu Africa ni Dikteta/
Uingereza Malkia amefikia muda wa kusepa/
Mule ndani kutamu bwana/
Watu wazima timamu kampeni wanalumbana/
Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa/
Ameniachia kifimbo Nyegere baba wa cypher/
Kifimbo ni hekima na busara/
Mwana anapaswa kutusikiza mafukara/
Makabwela na wanyonge kapuku wa hali duni/
Mlinda rasilimali hodari anayejali uchumi/
Kwa Mujibu wa sheria sheria ijibu/
Hatia inaishia uvumi nyumba si ya wahuni mnatia aibu/
Usiache shule soma choma vyeti vyako/
Ile nyumba ina mambo nyeti yaani zaidi ya nyeti zako/

Hook:
Kuna nini ndani ya ile nyumba mpaka mnagombea kuingia/Napagawa/
Pengine kuna dili za mavumba au labda ndio pepo ya Dunia/
Twende Sawa/