KIBABE LYRICS Artist: PROFESSOR JAY

KIBABE LYRICS
Artist: PROFESSOR JAY
Produced by Mr T touch
Verse 1.

Baada ya pilika na mheshimiwa spika ,
Mikumi imenipa kibali cha kuwakilisha,
Kick Kick Snare mmeniita nimeitika,
Now here comes the sound of the Mista Tongue Twister,
Mr MP, The MVP and the true definition of the Real Mc, ‘The Real Mc?
The Heavyweight Mc, Wanauzito wa Kinyoya now they wanna test Me,
The undisputed, Undefeated Mayweather,
Chaguo la kitaa naishi kwenye All weather,
Sometimes Chips KUKU, Sometimes Chukuchuku,
Wanadhani swimming pool nawaogesha kwenye Upupu, aaaaah
I shut em down na Onyo kwa makasuku,
Wenye fikra fupi kama umeme wa Luku,
Mi nawaza Billions wao wanawaza buku,
Ona wanavyoneng’eneka na hizi PUNCH zenye Muku,
The Motivator, Respect Mine , The True souldier,
Nimechonga barabara unapita the BULLDOZER,
The Icon tangu na tangu sio nguvu ya soda,
Huwezi fika Mia , kama hujaanza moja.

CHORUS:
Yeah Wanabeep wanakimbia, ONE MAN ARMY Wanapima wanakimbia, The ICON
Wanabeep wanakimbia,
Show KIBABE, FLOW za KIBABE, Style za KIBABE ×2

Verse 2.

Nakuchapa Kiuchumi, Nakuchapa kwa Ngumi, Nakuchapa kwa Heshima, Nakuchapa Kihuni,
Nakuchapa kwa Fanbase,
Hii ndio chata ya MIKUMI, Nakuchapa kwa Michano hata Urap kwa KIRUMI,
Nilishawasamehe wasanii wenzangu,
Waliokuja jimboni kupinga Ubunge wangu ,
Mabasi na Mabasi Jiongezeni wanangu,
Asante wana MIKUMI kwa kuwa na Imani kwangu,
Next time Mkija tena PROTECT YOUR NECK,
Msijesema sikusema it’s WAR for God’s sake,
Sanaa yataka umoja nitakubeba UKIANGUKA,
Hao wanawatumia na mwisho wanawatupa,
Kuingia Mjengoni hakujanitia MAWENGE,
Nimeongeza washkaji kina Mbatia na Chenge,
Vamia Nikulenge, Sio lazima Mnipende,
To all you Wack Mcs Nawakandia niwajenge,
Mbunge Ninayeongoza Binadamu na wanyama,
Bongo Flava MASIAH najua nachokifanya,
Usiponisikia Leo Jua kesho Narudi,
Mwambieni MFALME wenu seat yangu aifute vumbi.

CHORUS:
Yeah Wanabeep wanakimbia, ONE MAN ARMY, wanapima wanakimbia, THE ICON
Wanabeep wanakimbia
Show za KIBABE, Flow za KIBABE, Style za KIBABE ×2

BRIDGE:
Nimezaliwa kushinda eeeh
Na ndio maana niko Pale eeh
Anayepanga ni Mungu eeeh Binadamu hawezi bana eeeh
CHORUS.

Follow Twitter Tizneez
Facebook page Tizneez
Instagram Tizneez
Tuachie maoni yako hapa