KANUNI ZA HELA Lyrics By WAKAZI

12276764_368722089965026_1731402504_n

Verse:
Nipo kwenye game miaka mingi/Na kusaka hela, ndio kitu cha msingi/Uwe Kampuni uwe Msela/Lazima kuzingatia hizi kanuni Za hela/Namba MOJA, pesa sio kitu cha kungoja/Inabidi ulipwe instantly, tena mara moja/”Nilipe Nisepe”, Belle 9 alitoa hoja/Usiku uweke, ujikute unapewa noti forgery/MBILI, Lugha ya Taifa sio kiswahili/Ukiona mtu hakuelewi hebu toa laki Mbili/Yule anae endekeza ubahili Ni kama tu bubu/Ukishindwa kujieleza wajanja wanakusubu/TATU, pesa ya starehe haina mahesabu/ndio Maana hata asiye na mshahara bado anakula ulabu/Starehe gharama?! Well kama hujui Watu/Coz with only “50 Cents” you could be Ballin IN DA CLUB dude/NNE, I know you heard this before/Tumia hela ikuzoee bro/Namba TANO, Daima usikiuke makubaliano/maana wachimba chumvi hawashindwi kukutolea mfano/SITA, sahau mapenzi kwenye kitita/coz ukimkopesha Mpenzi kulipwa sahau kabisa/SABA, najua Hii wengine itawakwaza/mbele ya  pesa hupendwi mtu haijalishi hata maza/Aliyesema vizuri ni biggie niliyemkopi/Kamwe huwezi uka mix Damu na Noti/Namba NANE, tumia pesa Ili uweze Ku make money/ haujasikia, scared money don’t make no money/TISA, muhimu kuzingatia kabisa/Tumia hela kimahesabu sio Kisa umezishika/Kumbuka vipaumbele kabla kitaa hujatisha/ usije uza utajiri bila shilingi kulipwa/Namba KUMI, honestly, should have been number One/ unaweZa sahau kanuni zote ila hii tilia maanani/Wanasema, chezea mshahara usiichezee kazi/ no, cheza na Faida usichezee Mtaji/Fuata hizi Sheria, utakuwa milionea/na kama Tayari basi kamwe hutofulia/ila kumbuka pesa sio furaha Ya maisha/bali ni nyenzo muhimu, Kwa maisha kurahisisha/So ukileta tamaa uhai unaweZa hatarisha/wazee wa Kazi, Maisha yako kuyafupisha/hizi kanuni zinalenga ma hustler wa kila rika/ gotta go gotta go see, HELA zinaniita/whaaaat!!!
Outro:
Wajanja wa town wanakwambia kama hela hautoshi na unatakiwa ulipie kodi AU Gari, ni bora ulipie Gari maana “UNAWEZA KULALA KWENYE GARI ILA HUWEZI KUENDESHA NYUMBA”