Hapa Wakazi Tu (LYRICS)

VERSE 1
Nastahiki kufungiwa kimuziki kabisa/Kisa cha huyu msanii ni ka kisa cha Nabii Issa/Mbinguni nina hisa, with these bars/Hata nikioa Malaika, bado sitolewa sifa/Please God, not blasphemy comparin myself to Jesus/Let em ridicule, they did the same to Jesus/But Now we are all saved through Jesus/All you gotta say is in the name of Jesus/Subhanahu Wa Ta allah, ndo aliyenipa mitaaala/Na ujuzi, ili niweze kutawala kikufunzi/Lyrical Bruce Lee, teke Moja mnalala/Mnabaki teketeke, kwenye sekeseke hewala/I’m after real money, sio pesa za madafu/Hii harusi ya rap, hakuna keki wala ndafu/Bi harusi, ni beat honey, Nyuki na Siafu/Piga kazi ka Kiwavi iwe Moto au Barafu/
CHORUS
Napita mitaa ya Majumba sita,
Nikiuliza, je ni nani anaesikilizwa, wanajibu “Hapa Wakazi Tu”/Moja kwa moja mpaka Sinza, mpaka Mwenge nikiuliza, jibu ni “Hapa Wakazi Tu”/Nachosikia kwenye spika, Mbagala na Temeke, Chang’ombe mpaka Tandika “Hapa Wakazi Tu”/Kinondoni na Ilala, Migomigo, Ubungo mpaka Kimara jibu ni “Hapa Wakazi Tu”/
VERSE 2
Wakongwe wanadai, tulia we bado Dogo/Na mi nawaambia, kimuziki ni kama Dogo/Nachofanya hamuwezi, huu  Uwendawazimu/Ndo maana kwenye midundo mi nadunda ka Hashim/Metaphorically, lugha ya picha/Zaidi ya Kiranja, lyrically nawafundisha, KRS the teacher/Tofautisha Sanaa na biashara ya muziki/I do both, natisha, kivipi useme Rap haiuziki/I said I’m bilingual, wakanibeza/Sasa kila rapper bongo, ana flow kwa Kiingereza/Je nikutoka international au kugeza/But it ain’t my fault, see ya still can’t see me, kwa makengeza/Y’all Cross eyed, as I dissect, these cross lines/Live and direct, no cosigns, on the cross lies/Your ass, confess that I’m one of the best/Of all times, and in no time, My guess, I’ll be in your top 5/
VERSE 3
Mpende akupendae, asiyekupenda achana nae/We humpendi Wakazi, wenzako jukwaani wanachana nae/Mstari kwa mstari, bar for bar/Wanamfanya anang’aa, rappers wengine wame fubaa/Haya maisha sio visa vya Adili na nduguze/Kisa ulisha rap awali, ndio ufanye tukutukuze/Hii sio Misa ya Kanisa, nawalisha muziki/Naskika kitaa, bila kiki, freestyle hata ka Redioni siskiki/Mashabiki, hebu jipeni shavu/Japo Kiroba, ingawa usawa mbovu, zama za Magu/We gon pop bottles nikisha tikisa nyavu/Jabulani, Ila kwa sasa kila skani nachotaka kusikia ni “Hapa Wakazi Tu”
OUTRO
Singida Dodoma/
Iringa Kigoma/
Mwanza Shinyanga/
Mbeya na Tanga/
Arusha Na Mara/
Bukoba Mtwara/
Moshi na Moro/
Njombe na Lindi/
Rukwa na Ruvuma /
Pemba na Unguja/
International mpaka local, Wakazi swagga bovu in here laying the vocals.
Hata haters ukiwauliza nani wanae mchukia kuliko wote, jibu ni Hapa Wakazi Tu.

Attachment