ENZI ZA UTOTO Lyrics by SONGA

index

Nilizaliwa kwa Mama peke yangu,
sikujua kama ningekutana na wenzangu,
wazazi kisha ndugu,
Mwisho nikajua aliyefanya haya yote ni Mungu,
Sasa akili ikachachamaa,
na hiyo ni baada ya kukutana na rafiki kadhaa,
ambao wengi tuliishi kwa mtaa,
tukibadili mazingira na jinsi ya kukaa,
Huku kichwani utoto umetanda,
nikifanya kosa nakula viboko mixer mkanda,
Kipindi hicho hata sijaanza ku rap,
nikichelewa home nnaweza nikapigwa hata na kiatu,
Sebule disco jirushe kwenye makochi,
ila ukikutwa unaweza ukajuta kwa hayo makofi,
tena beki alivyo mnoko,
Ukifanya soo ye ndo atakusaka kila chocho.

2nd Verse

Kumbuka ni kitambo kabla ya Mister Nice na Takeu,
zishakuja sana kesi nimemtoa mtu ng’eu,
Nilikuwa situlii akija mgeni,
labda uniwekee movie ya Bruce Lee au Jackie Chen,
Majirani waliniona ni mtoto hatari,
usiku napiga kelele mithili ya popo hawalali,
mwendo wa vurugu narusha makopo juu ya dari,
nikitulia juwa ni siku ya ndondo na wali,
Ikipita sana muda sijanywa soda,
najifanya naumwa unaweza hisi nimelogwa,
nakunja sura sitaki kupiga soga,
nakuwa sana mbishi likija suala la kuoga,
Muda mwingine nazuga hakuna sabuni,
kumbe nimeificha ili nicheki cartoon,
Mtoto wa uswazi sijui midoli wala toy,
kila siku inaisha nambonji nikiwa hoi.

ENZI ZA UTOTO.