Professor Jay (Bio)

Prof-Jay

Joseph Haule (amezaliwa tar. 29 Desemba 1975) ni msanii wa muziki wa hip hop laini kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Professor Jay. Katika Tanzania, Prof. Jay anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee waweze kusikiliza muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew – Chemsha Bongo. Professor Jay anatokea kundi la Hard Blasters Crew. Kundi hili ni moja ya makundi yaliyofanya muziki huu ambao hujulikana kama ‘muziki wa kizazi kipya’ kukubaliwa na sehemu kubwa ya wa Tanzania.

Maisha ya muziki

Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 90 hivi na alijiunga na kundi la ‘Hard Blasters Crew‘(HBC) mnamo mwaka 1994. Mwaka 1995 Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini Tanzania. Jay na HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo ‘Funaga Kazi’ mwaka 2000 Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania. Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama ‘Chemsha Bongo’ na ‘Mamsapu’ ambazo zilichangia kufanya muziki wa ‘Bongo Flava‘ kuwa wa kila rika na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huu ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni

Msanii Binafsi

Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo 2001 na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo “Machozi Jasho na Damu”. Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya Prof. Jay kupata tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa nyimbo yake ya ‘Ndio Mzee’ kutoka kwenye albamu hiyo. na ikifuatiwa na Nyimbo ya “Piga Makofi na Bongo Dar es Salaam

Mwaka 2003 Alitoa albamu ya pili iitwayo “Mapinduzi Halisi” ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya Muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii imebebanNyimbo kama “Zali la Mentali”, “Msinitenge,” na “Promota Anabeep”

Mwaka 2006 Januari alitoa albamu ya tatu iliyoitwa “J.O.S.EP.P.H”. Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka Mwanzo kabla ya Albamu kutoka. Nyimbo hii ilichaguliwa kuwa nyimbo bora ya Bongo Flava kwenye BBC na Radio One Awards.

Mpya imewahi kuteuliwa kuwa ni albamu bora ya Hip Hop , Mtunzi bora wa nyimbo za Hip Hop, na Nyimbo bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. 2006.”Nikusaidieje”. na Baadae Kisima Music Awards ya Kenya ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania.

Albamu

Tuzo Alizopata

Wasanii alioshirikiana nao kimuziki

Lady Jay Dee. ( Bongo Dar es Salaam na Nimeamini)

Mc Babu Ayubu. ( Ndio Mzee )

Juma Nature. ( Ndio Mzee na Zali la Mentali )

Q Chilah. ( Msinitenge )

Inspector Haroun. ( Hakuna Noma )

Simple X. ( Piga Makofi na Hakuna Noma )

Jose Chameleone. ( Ndivyo Sivyo – Kutoka Uganda )

Adili a.k.a Hisabati

Mwana FA (ni jukumu letu)

Albert magweir (Una)

Mr II sugu (Inatosha)

Ngoni (Mapinduzi)

Jay mo (Tathimini)

Ferooz (Zubeda)

Mkoloni (Promota anibeep)

Diamond Plutnum (Kipi sijasikia)